Monday, February 02, 2015

NAIBU MTENDAJI MKUU PDB/BRN ATAKA MAAFISA KILIMO KUWA WABUNIFU


Naibu Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango wa BRN, Bw. Peniel Lyimo akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi na maafisa kilimo kilichoanza Dar es Salaam leo Jumatatu ambapo aliwataka kuwa wabunifu, kutatua changamoto za kisekta na kushirikishana na wataalamu wengine ili malengo ya BRN katika kilimo yafanikiwe.
Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika Wizara ya Kilimo, Bw. January Kayumbe akitoa mada kuhusu malengo na utekelezaji wa BRN katika sekta ya kilimo kwa washiriki kutoka mikoa inayotekeleza BRN katika kilimo (hawapo pichani).
Sehemu ya mada ikiainisha eneo mojawapo ambapo BRN iliweka mikakati katika sekta ya kilimo ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa maghala 275 kwa ajili ya kuhifadhi mazao nchi nzima. Taarifa ya utekelezaji wa mwaka mmoja tu ikionesha kuwa maghala yote yameshafanyiwa tathmini na ujenzi na ukarabati wa baadhi ukianza.

Sehemu ya maafisa wa ngazi mbalimbali katika sekta ya kilimo kutoka mikoa inayoshughulika na kilimo chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) wakifuatilia hotuba ya Naibu Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango huo, Bw. Peniel Lyimo (hayuko pichani) wakati wa kikao kazi kilichoanza Dar es Salaam jana.
Washiriki wa kikao kazi kilichoanza leo Dar es Salaam wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa kujadili namna ya kuboresha zaidi utekelezaji wa miradi ya BRN katika sekta ya kilimo. (Picha na Idara ya Mawasiliano PDB)

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...