Wednesday, September 03, 2014

SHIRIKA LA NYUMBA TANZANIA (NHC) LAKARABATI SHULE YA HASSANGA JIJINI MBEYA

 Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas  Kandoro akikata utepe kuzindua ukarabati wa Madarasa manne na Jengo moja la Utawala katika Shule ya Msingi Hasanga uliofanyika leo Uyole Mbeya.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas  Kandoro, viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa Tanzania (NHC), Viongozi wengine wa Serikali na Walimu wa Shule ya Msingi ya Hasanga wakifurahia Baada ya Kuzindua Rasmi ukarabati wa ujenzi huo.
Meza kuu
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akizungumza na wananchi, wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi ya Hasanga katika Sherehe ya kukabidhi Majengo ya Shule hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Mchechu akizungumza jambo wakati wa Sherehe hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigallah King akimkaribisha Mkuu wa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro
Meya wa Jiji la Mbeya Atanus Kapunga akitoa neno la Shukurani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Akiwakaribisha Wageni katika Sherehe hizo
Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Mbeya Anthony Komba akisoma Taarifa ya ukarabati wa Shule hiyo
 Mwalimu Neema Sanga (Kushoto) akisoma  Risala ya Shule 
Baadhi ya Wageni waalikwa na Meza Kuu
 Baadhi ya Wanafunzi na Wazazi 
Wanafunzi wakiimba Ngonjera 
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Abbas Kandoro Akiendesha Harambee
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikagua Baadhi ya Majengo
Muonekano wa Baadhi ya Majengo ya Shule ya Msingi Hasanga yaliyokarabatiwa na Shirika la Nyumba la Taifa 
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua tukio.

SHIRIKA la Nyumba la Taifa(NHC) limefanya ukarabati wa majengo ya shule ya Msingi Hassanga iliyopo Uyole jijini Mbeya ambayo alisoma Mkurugenzi Mkuu Nehemia Mchechu.
Makabidhiano ya mradi huo umefanyika leo katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na Mkurugenzi mkuu, viongozi wa Halmashauri ya Jiji, Wilaya na Shirika la Nyumba ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alikuwa mgeni rasmi.
Aidha ukarabati wa majengo manne na jengo moja la utawala uliofanywa na shirika la Nyumba(NHC) umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 31.
Mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu,katika taarifa yake iliyosomwa na Meneja wa Shirika hilo Mkoa wa Mbeya,Antony Komba, amesema Shirika hilo liliamua kufanya ukarabati wa jengo la utawala na madarasa manne ya shule hiyo kama sehemu ya mchango wake kwa jamii kufuatia maombi yaliyofanywa na Kamati ya shule ya kuombwa ukarabati wa majengo hayo.
Amesema kazi ya ukarabati ilianza Aprili 19 na kukamilika Agosti 20, Mwaka huu ambapo Shirika lilikarabati Jengo la utawala katika ujengaji upya wa kuta za jengo , bimu na uezekaji upya wa paa, upigaji lipu, sakafu na rangi pamoja na kuweka milango na madirisha ya alminium kwa gharama ya shilingi Milioni 22,77,900.
Ameongeza kuwa ukarabati katika madarasa manne ulihusu upigaji upya wa lipu ukutani, utengenezaji wa sakafu , utengenezaji wa shata za madirisha pamoja na upakaji rangi uliogharimu shiringi Milioni 8,803,000 na kufanya jumla ya shilingi Milioni 31, 577,900.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, mbali na kulishukuru shirika hilo kwa msaada wao huo pia ametoa wito kwa Wanafunzi na Walimu pamoja na uongozi wa kamati ya shule kuyatunza majengo hayo ili yaweze kudumu.
Hata hivyo katika hatua Nyingine Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alilazimika kuendesha harambee nyingine baada ya Mkurugenzi wa NHC, Mchechu kujibu risala ya walimu walioomba kukarabatiwa majengo mengine ambapo alisema kama wataweza kuchangia chochote Shirika litaweza kumalizia.
Katika harambee hiyo ambayo pia ilichangiwa na Shirika Mkuu wa Mkoa alifanikiwa kukusanya Shilingi Milioni moja na laki tatu ambazo alizikabidhi kwa Mkurugenzi wa Shirika ambaye baada ya kupokea aliahidi kuanza ujenzi kesho wa majengo mengine manne.
Nao Walimu wa Shule ya Msingi Hassanga katika Risala yao kwa Mgeni rasmi,iliyosomwa na Mwalimu Neema Sanga, wamelipongeza shirika la Nyumba kwa kukarabati majengo hayo.
Wamesema ukarabati wa Vyumba vine vya madarasa, ofisi ya Walimu pamoja na Ofisi ya Mwalimu Mkuu ni moja ya kutambua umuhimu wa Elimu na kujenga mazingira rafiki ya kufundisha na kujifunzia.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...