Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu imemteua Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania Agustino Ramadhan kuwa rais wa mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka miwili uteuzi huounaanza mara moja baada ya aliyekuwa rais wa mahakama hiyo Sophia Akuffo wa Ghana kumaliza muda wake.
Jaji Ramadhani Mtanzania wa kwanza kushikilia kiti hicho tangia kuanzishwa kwa mahakama hiyo baada ya kupata kura 7 kwa kura nne dhidi ya mpinzania wake katika nafasi hiyo ya rais wa mahakama hiyo huku nafasi ya makamu wake ikichukuliwa na jaji Eisie Thompson kutoka nchi ya Nigeria.
Katika nafasi hiyo ya makamu walikuwepo majaji watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo na baada ya upigaji wa kura mara ya kwanza wawili walifungana kwa kura 4 na mmoja kupata kura tatu ndipo uchaguzi ulirudiwa na jaji Thompson kuibuka mshindi kwa kupata kura 6 dhidi ya tano za mpinzani wake.
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya uteuzi huo jaji Ramadhan alisema kuwa ni heshima kwa Taifa la Tanzania kwani ndio mara yake ya kwanza kupata nafasi hiyo huku akisema kuwa nafasi hiyo ni heshima kwake na kwa taifa lake.
“Kesi yeyote inayohusu nchi yangu mimi sitakuwepo kutokana na sheria zetu za mahakama hii na kuwa tayari watanzania watano wamefungua kesi kwenye mahakama hii na kesi mbili zimetolewa hukumu ya mchungaji mtikila na Zongo”alisema jaji Ramadhan
Alisema kuwa mpaka sasa ni kesi 5 zimefunguliwa katika mahakama hiyo na mbili teyari zimetolewa ikiwemo dhidi ya serekali ya Tanzania kesi iliyofunguliwa na mchungaji Christopher Mtikila iliyohusu mgombea Binafsi huku akisema kuwa kuchukuwa hatua kwa utekelezaji wa hukumu kunategemea na serekali kama imejiunga na mikataba ya kimataifa.
Alitanabaisha kutokana na sheria za mahakama hiyo wakati wa usikilizaji wa kesi zinazoihusu nchi yetu yeye hawezi kuisikiliza na kuwa Atajitoa kuisikiliza kama shiria ilivyo ya mahakama hiyo huku akisema mahakama hiyo inaundwa na majaji 11 kutoka nchi tofauti za bara hili .
Aidha mahakama hiyo iliwaapisha majaji watatu wa mahakama hiyo kabla ya kuanza mchakato wa upigaji kura kumteuwa jaji wa mahakama hiyo huku ripoti ya mahakama hiyo kila mwaka ikipelekwa kwa umoja wa nchi za Afrika.
Uchaguzi huo huwa ni vipindi vya miaka miwili miwili na iwapo ukimaliza muhula wa kwanza kama utateuliwa tena kushika nafasi hiyo utakuwa ndio kipindi chako ya mwisho kushikilia nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment