Monday, September 29, 2025

WASTAAFU KUPATA HUDUMA MAALUM ZA KIBENKI NA BIMA


Baadhi ya wastaafu na wataalam wa kifedha wakimsikiliza Meneja Mwandamizi wa Mauzo wa Benki ya Stanbic, Priscus Kavishe kwenye kongamano la wastaafu lililoandaliwa na Benki ya Stanbic Tanzania lenye lengo la kutoa huduma za kifedha na bima kwa wastaafu nchini. Kongamano hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.


…………….

Dar es Salaam, Septemba 26, 2025 – Wastaafu na wale wanaokaribia kustaafu nchini Tanzania wamehimizwa kujikita katika mipango thabiti ya kifedha, huduma za bima na uwekezaji ili kujihakikishia maisha yenye heshima na ustawi baada ya kumaliza muda wao wa kazi.

Ujumbe huu ulikuwa lengo kuu la Mkutano wa Wastaafu ulioandaliwa na Benki ya Stanbic, ambao uliwakutanisha wastaafu, wataalam wa kifedha na wadau wa sekta mbalimbali kujadili mbinu kwa vitendo ili kujiandaa kimaisha baada ya kustaafu. Tukio hili ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya Benki ya Stanbic nchini Tanzania, yenye kaulimbiu ‘Miaka 30 ya Kukua Pamoja.’

Mjadala ulijikita zaidi katika akaunti ya Hekima Banking, akaunti maalumu iliyoanzishwa na Stanbic kwa ajili ya watu wenye umri wa miaka 55 na kuendelea. Akaunti hii inawapa wastaafu urahisi wa kufanya miamala, kuweka akiba, kupata mikopo na ushauri wa kifedha na uwekezaji.

Kwa mujibu wa Priscus Kavishe, Meneja Mwandamizi wa Mauzo wa Benki ya Stanbic, mpango huu umetengenezwa ili kuwapa wastaafu usalama na fursa. “Kwa Stanbic Bank, tunaamini kustaafu si mwisho, bali ni mwanzo wa fursa mpya. Kupitia Hekima Banking, tunawapa wastaafu suluhisho za vitendo zitakazowawezesha kuishi kwa heshima, kuwekeza na kuendelea kuchangia kwa maana katika familia na jamii zao,” alisema Kavishe.

Akaunti ya Hekima haina ada za kila mwezi, haina salio la chini, inapatikana kwa sarafu mbalimbali, na inatoa huduma za kidigitali saa 24/7. Wastaafu pia wanaweza kupata mikopo hadi TZS milioni 80 kwa masharti nafuu, huku mafao ya pensheni yakitumika kama dhamana. Aidha, wastaafu wanaweza kuomba bima ya afya pamoja na bidhaa nyingine za bima.

Umuhimu wa bima katika maisha ya kustaafu ulisisitizwa na Naphtal Ntangeki, Afisa wa Bima Stanbic, aliyebainisha kwamba bima ni nguzo muhimu ya mpango wa kifedha. “Kustaafu kwa usalama hakujengwi kwa akiba pekee. Bima inawapa wastaafu ujasiri wa kupanga maisha yao ya baadaye bila hofu ya misukosuko ya kifedha. Kwa Stanbic, tunaunganisha bima katika suluhu zetu ili wastaafu waweze kuishi miaka yao ya baadaye kwa uthabiti na heshima,” alisema Ntangeki.

Washiriki wa mkutano huo walipongeza hatua hii, wakibainisha kuwa imewapa maarifa na mbinu za moja kwa moja. Michael Liymbo kutoka KPMG, aliyeshiriki mkutano huo, alieleza tukio hilo kuwa na manufaa makubwa. “Mkutano wa leo umenifumbua macho. Nimejifunza jinsi akaunti ya Hekima Banking na huduma za bima zinavyoweza kusaidia wastaafu siyo tu kulinda fedha zao, bali pia kuishi maisha yenye heshima. Hatua hii ya Benki ya Stanbic kwa kweli inawanufaisha wataalamu na wastaafu wa baadaye,” alisema Liymbo.

Mkutano wa Wastaafu ni sehemu ya shughuli za mwaka mzima za Stanbic kuadhimisha miaka 30 ya shughuli zake nchini Tanzania. Zaidi ya kusherehekea historia yake, benki inatumia fursa hii kuanzisha suluhisho zinazooana na malengo ya Taifa ya Vision 2050 ya kukuza ujumuishaji wa kifedha, uthabiti na kuboresha maisha ya wananchi wote.

No comments:

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Rugambwa wapokelewa Bukoba

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, aliyefariki hivi karibuni, uliwasili leo katika Kanisa Kuu la Bikira Maria wa Huruma, Jimbo Ka...