Sunday, September 28, 2025

MRADI WA TACTIC KUBDIDLISHA TASWIRA YA MANSPAA YA MOSHI-NURDIN BABU









 Ataka Kasi na Ubora katika utekelezaji wake 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Hassan Babu amesema ni matarajio yake kuwa utekelezaji wa mradi wa uendelezaji Miji Tanzania TACTIC kwa Manispaa ya Moshi utaleta mabadiliko chanya kwa wananchi na wageni ambao watafaidi huduma za usafiri na usafirishaji pamoja na mazingira bora ya shughuli za kiuchumi kwa kuongeza thamani ya maeneo na kukuza pato la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

Mkuu huyo wa Mkoa ameyaeleza hayo mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa ujenzi wa Miradi ya TACTIC katika Manispaa ya Moshi leo Septemba 27, 2025 kwenye Viwanja vya shule ya Msingi Msaranga, mradi ukihusisha ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya barabara, mitaro ya kutiririsha maji ya mvua pamoja na jengo la usimamizi, vyote vikigharimu Shilingi Bilioni 22.9.

"Jukumu letu ni kuitunza miundombinu hii itakayojengwa kwa gharama kubwa ili iweze kudumu kwa muda uliotarajiwa. Nitoe Rai kwa Mkandarasi kuhakikisha kazi hii inafanyika kwa haraka, ubora uliokusudiwa na kukamilika kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na miundombinu hii ambayo Serikali imewekeza katika Manispaa yetu." Amenukuliwa akisema Mhe. Babu.

Katika maelezo yake, Mhe. Babu amemuagiza Mkurugenzi Mkuu na Mameneja wa TARURA pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Moshi kusimamia kikamilifu miradi hiyo kwa kutumia rasilimali watu na vifaa vilivyopo, akitaka Mkandarasi kupewa ushirikiano wa karibu kwa kuzingatia muundo wa utekelezaji wa mradi wa TACTIC unaojumuisha wataalamu wa pande zote.

Babu ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikichukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi kwa kupitia miradi mbalimbali ikiwemo TACTIC yenye kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, ujenzi wa masoko na vituo vya Mabasi pamoja na utunzaji wa mazingira.

Jumla ya Gharama ya mradi huo ikiwa ni Dola za Marekani Milioni 410, ikitekelezwa kwenye Miji 45 ya Tanzania

No comments:

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Rugambwa wapokelewa Bukoba

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, aliyefariki hivi karibuni, uliwasili leo katika Kanisa Kuu la Bikira Maria wa Huruma, Jimbo Ka...