Monday, September 29, 2025

TANAPA YASHIRIKI MAPOKEZI YA MWANARIADHA BINGWA WA DUNIA SAJINI TAJI SIMBU - ARUSHA.










Na. Jacob Kasiri - Arusha

Leo Septemba 29, 2025 TANAPA imeshiriki hafla ya mapokezi ya Bingwa wa Dunia mbio ndefu (Marathon) kilometa 42  Sajini Taji Alphonce Simbu yaliyofanyika  takribani wiki mbili jijini Tokyo - Japan, mapokezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege Kisongo jijini Arusha.

Katika mapokezi yaliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), SGT Simbu aliwashukuru TANAPA kwa kushiriki mapokezi hayo na kumuandalia gari alilotumia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa maandalizi ya filamu ya “Tanzania:The Royal Tour”.

Simbu aliongeza kuwa licha ya heshima aliyoipata duniani ya kushinda medali ya Dhahabu katika mbio hizo za km 42, pia TANAPA imempa heshima isiyo kifani kutumia gari aliyotumia Mkuu wa nchi kama filamu yake iliyojizolea umaarufu ndani na nje ya Taifa letu.

Wakati wa kuhitimisha hafla ya mapokezi hayo yaliyofanyika katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.

No comments:

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Rugambwa wapokelewa Bukoba

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, aliyefariki hivi karibuni, uliwasili leo katika Kanisa Kuu la Bikira Maria wa Huruma, Jimbo Ka...