Sunday, September 28, 2025

πŸ“*TAWA YAADHIMISHA SIKU YA UTALII DUNIANI NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM







Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imeadhimisha Siku ya Utalii Duniani kwa kuwapeleka makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo watoto wenye mahitaji maalum na wanafunzi kutembelea Hifadhi ya Wamimbiki iliyopo katika Mikoa ya Morogoro na Pwani kwa lengo la kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.

Makundi hayo yamejumuisha, Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Dar Ul Muslimeen pamoja na Shule za Msingi na Sekondari za Gwata,Maseyu,Kitungwa, Migogodo na Kivuge zilizopo Mkoani Morogoro.

Sambamba na hilo, TAWA imeendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa watalii hao ili kujenga kizazi kinachopenda uhifadhi na utalii kwa ajili ya kuwa na Utalii wenye mageuzi na maendeleo endelevu.

Siku ya utalii duniani inaadhimishwa kila tarehe Septemba 27 na kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo *Utalii na Mageuzi Endelevu*.

No comments:

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Rugambwa wapokelewa Bukoba

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, aliyefariki hivi karibuni, uliwasili leo katika Kanisa Kuu la Bikira Maria wa Huruma, Jimbo Ka...