Sunday, September 28, 2025

RAIS SAMIA ANATHAMINI MCHANGO WA WAONGOZA WATALII NCHINI









Na Mwandishi Wetu- Karatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anathamini na kujua kazi na mchango wa waongoza watalii nchini Tanzania.

Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi ameyasema hayo katika tukio  la Fainali ya Safari Field Challenge Toleo la 10, likiambatana na maadhimisho ya Miaka 10 ya mashindano haya, sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani lililofanyika kwenye ukumbi wa Oasis Wilayani Karatu, Arusha usiku wa Septemba 27,2025.

“Rais Samia anafahamu tunafanya tuzo hapa leo na ameangalia challenge zote mlizofanya na amekubali na akasema anawapenda sana na anawaelewa sana na ndio maana alifanya filamu ya Tanzania the Royal Tour, alikwenda pemba akuvua Samaki” amesema Dkt. Abbasi.

Aidha, Dkt. Abbasi ametumia fursa hiyo kuwahimiza waongoza watalii kushiriki katika tuzo za utalii na uhifadhi zinazotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025.

“Tumezindua tuzo za utalii na uhifadhi, ni tuzo za ushindani watu watashindanishwa kwenye kategoria mbalimbali hivyo mshiriki katika kupambania kategoria mbalimbali ikiwemo ya safari guid, mountain guide n.k” amesema Dkt. Abbasi.

Amesema kuanzi tarehe 10 mwezi Oktoba tuzo zitafunguliwa na  zitakuwa na kategoria saba zenye tuzo zaidi ya 56, na tarehe 19 itakuwa ni usiku wa tuzo.

No comments:

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Rugambwa wapokelewa Bukoba

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, aliyefariki hivi karibuni, uliwasili leo katika Kanisa Kuu la Bikira Maria wa Huruma, Jimbo Ka...