Monday, September 29, 2025

REA yauza majiko 1,500 kwa bei ya ruzuku kwenye maonesho ya Madini Geita



๐Ÿ“ŒREA yapongezwa kwa kuuza majiko kwa bei ya ruzuku na kutoa elimu ya miradi ya wakala

๐Ÿ“Geita

Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita yamehitimishwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambayo yalifunguliwa Septemba 18 na kufikia kilele tarehe 28 Septemba, 2025

Wakala umeshiriki maonesho hayo kwa kutoa elimu ya nishati safi ya kupikia, kutoa elimu ya miradi inayotekelezwa na wakala wa nishati vijijini pamoja na fursa zinazopatikana kwa wakala kama vile vituo vidogo vya mafuta.

Sambamba na hayo Wakala unahamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuuza kwa ruzuku mitungi ya gesi ya kilo 6 ambayo inauzwa kwa bei ya 50% ambayo ni kiasi cha shilingi 17,500 ambapo jumla ya mitungi 5,00 imeuzwa kwa ruzuku kwenye maonesho.

Pamoja na hayo, Wakala unafadhili uuzwaji wa majiko banifu yanayotumia mkaa mbadala pamoja na mkaa wa kawaida, majiko hayo yameuzwa kwa bei ya ruzuku ya 85% ambayo ni shilingi 6,195 ambapo bei yake ya kawaida ni shilingi 41,300 ambapo majiko banifu 1,000 yatauzwa kwa bei ya ruzuku katika maonesho hayo. 

Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini 2025  yamefanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita.

No comments:

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Rugambwa wapokelewa Bukoba

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, aliyefariki hivi karibuni, uliwasili leo katika Kanisa Kuu la Bikira Maria wa Huruma, Jimbo Ka...