Friday, September 26, 2025

NGORONGORO YANADI FURSA ZA UTALII NA UWEKEZAJI ULAYA



Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma za Shirika Ngorongoro, Bw. Aidan Makalla (kulia), akiwa ameambatana na Abdiel Laizer, Afisa Utalii Mkuu Msaidizi, amekutana na mawakala mbalimbali wa utalii kunadi fursa za utalii na uwekezaji zilizopo Ngorongoro katika maonesho ya “My Tanzania Roadshow 2025 Europe”.

Maonesho hayo yanafanyika kuanzia Septemba 22 hadi 27, 2025 katika miji ya Stuttgart – Ujerumani, Salzburg – Austria, Ljubljana – Slovenia na Milan – Italia.

Tukio hilo linaratibiwa na Kampuni ya KILIFAIR na ni jukwaa la kipekee la kutangaza vivutio vya utalii, kuibua fursa mpya za uwekezaji na kuitangaza Tanzania kama kitovu cha utalii katika soko la Ulaya.

Ngorongoro, ikiwa ni moja ya hazina kubwa za malikale na urithi wa dunia, imeendelea kuwa kivutio cha pekee kinachochangia kwa kiasi kikubwa mapato ya taifa kupitia sekta ya utalii.

 Kwa kushiriki maonesho haya, Shirika la Hifadhi la Ngorongoro linaimarisha nafasi yake kimataifa kwa kuwavutia wawekezaji na kuendeleza mikakati ya kuongeza idadi ya watalii kutoka bara la Ulaya.

No comments:

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Rugambwa wapokelewa Bukoba

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, aliyefariki hivi karibuni, uliwasili leo katika Kanisa Kuu la Bikira Maria wa Huruma, Jimbo Ka...