Katika kesi
hiyo ya jinai namba 275 ya mwaka 2022 imetolewa hukumu leo na Hakimu
Mkazi Mfawidhi, Isihaka Kupwa ambapo Msama alikuwa anakabaliwa na
mashtaka matano.
Hakimu Kupwa alisema mahakama hiyo ilipokea na kupitia vielelezo na ushahidi wa pande zote mbili pasina kuacha.
Hakimu
Kupwa amesema baada ya mahakama hiyo kupitia ushahidi wa pande zote
mbili, imeona upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi
yake hivyo inamuachia huru na kumpa ushindi.
Miongoni kwa sababu
alizozitaja Hakimu Kupwa ni kwamba Jamhuri ilishindwa hata kuwasilisha
cheti cha kifo cha marehemu aliyetajwa katika kesi hiyo, pia kukosekana
kwa mtaalamu wa kuthibitisha maandishi yaliyoghushiwa.
“Mahakama hii inamuachia huru Alex Msama Mwita, haki ya kukata rufaa ipo wazi,”.
Miongoni
mwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili Msama ni Kughushi, ambapo anadaiwa
siku isiyojulika ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kufanya
udanganyifu alighushi nyaraka za mauziano yenye Tarehe ya Julai 6, 1970,
akikusudia kuonyesha kuwa ni nyaraka halisi za mauziano kati ya Khalid
Swalee Chengu na Ndelikyama Mweleli huku akijua fika kuwa ni za uongo.
Pia
shtaka jinginr inadaiwa Aprili 24, 2016 ndani ya Jiji la Dar es Salaam
Kwa nia ya kufanya udanganyifu, anadaiwa kughushi sahihi ya Ndelikyama
Mabolio Mweleli katika Mkataba wa mauzo wa Aprili 24, 2016 Kwa kusudi la
kuonyesha kuwa ni nyaraka halisi za mauziano kati yake na Ndelikyama
Mabolio Mweleli, huku akijua wazi kuwa ni uongo.
Pia inadaiwa
siku ya Aprili 24, 2016 ndani ya Jiji la Dar es Salaam, Kwa nia ya
kufanya udanganyifu, alighushi barua ya ofa yenye kumbukumbu namba
D/KN/A/13504/TMM yenye Tarehe ya Septemba 28, 1979 na jina la Ndelikyama
M. Mweleli, Kwa kusudi la kuonyesha kuwa Kiwanja namba 160 kilichopo
Mbezi Beach Dar es Salaam, kilikuwa ni Cha Ndelikyama Mabolio Mweleli
huku akijua wazi kuwa ni za uongo.
Wednesday, January 01, 2025
MAHAKAMA YAMUACHIA HURU ALEX MSAMA
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kivukoni Kinondoni imemuachia huru Mkurugenzi wa Msama
Promotion, Alex Msama baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha
mashtaka ya kughushi nyaraka za kiwanja dhidi yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Dkt Kikwete Akoshwa na Ushiriki wa Wadau Binafsi Kwenye Miradi ya Maendeleo, Aipongeza Benki ya NBC
Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) akikabidhi tuzo maalum kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pil...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment