Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameongoza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa kutembelea Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ili kukagua maendeleo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025.
Ukumbi huo, wenye uwezo wa kuchukua takriban watu 3,000,
unakarabatiwa kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha mazingira bora kwa
mkutano huo muhimu. Mkutano huu utakuwa na agenda kadhaa, ikiwemo
kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), kufuatia kujiuzulu kwa
Komredi Abdulrahman Kinana mwaka jana.
Balozi Nchimbi, akiwa ameambatana na Manaibu Katibu Mkuu wa CCM, John
Mongella (Bara) na Dkt. Mohamed Said Dimwa (Zanzibar), pamoja na wajumbe
wa Sekretarieti, alishuhudia kasi kubwa ya maandalizi hayo, huku
akiwapongeza wahusika kwa jitihada zinazofanywa kuhakikisha kila kitu
kinakuwa tayari kwa wakati.
No comments:
Post a Comment