Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla,
MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) unatarajia kufanyika Januari 18 hadi 19 mwaka huu ukiwa na ajenda
tatu ikiwemo kuziba nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.
Akizungumza
na waandishi wa habari Makao Makuu ya CCM katika ukumbi wa White House
jijini Dodoma leo, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos
Makalla, amesema mkutano mkuu huo utakuwa na ajenda tatu.
Alizitaja
ajenda hizo hizo ni kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara
kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Ndugu Abdulrahman
Kinana,kupokea kazi za Chama kuanzia mwaka 2022 hadi 2025 pamoja na
kupokea taarifa ya utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Ameeleza
kuwa taarifa hizo za utekelezaji ilani ni kutoka Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)
Kuhusu
mchakato wa kumrithi Kinana, amesema mrithi wa nafasi hiyo anatarajiwa
kupatikana baada ya kamati kuu kuwasilisha mapendekezo ya jina kwa
halmashauri kuu kisha halmashauri kuu kuwasilisha jina hilo kwa wajumbe
wa mkutano mkuu kwa ajili ya kupigiwa kura.
"Kumekuwa na uvumi,
unaona vichwa vya habari kwamba CCM patashika, wafuatao watajwa kurithi
nafasi ya Kinana, nani kati ya hawa atachukua nafasi ya Kinana, wengine
wanakwenda mbali kuandika wafuatao kuchukua nafasi ya Kinana. Kila mmoja
anaandika navyotaka.
"Nataka kusema kwamba, nafasi ya Makamu
Mwenyekiti haigombewi, unaposema kinyang'anyiro kinatoka wapi wakati
nafasi haigombewi wala haijazwi fomu?," alieleza.
CPA Makala
alisisitiza: "Tutampata makamu mwenyekiti baada ya mapendekezo ya kamati
kuu na halmashauri kuu, kisha jina la atakayeziba nafasi hiyo
litawasilishwa katika mkutano kuu na hapo ndipo zitapigwa kura ya ndiyo
au hapana."
"Hatukuwa kimya, Chama kinaongozwa kwa katiba, kina
utaratibu wake, hatuwezi kuongozwa kwa hisia za watu. Kwa sasa Kamati
Kuu imeona ndiyo muda muafaka kujaza nafasi hiyo," alisema.
CPA
Makalla aibainisha kuwa mkutano mkuu utatanguliwa na vikao vya Kamati
Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, vinavyotarajiwa kufanyika Januari 16
mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZISHI YA MWENYEKITI WA ZAMANI WA CCM LIWALE
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika mazishi ya Mwenyekiti wa zamani w...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment