Sunday, January 12, 2025

Rais Samia Aungana na Watanzania Kuadhimisha Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanMhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 12 Januari, 2025, ameungana na wananchi wa Zanzibar kusherehekea kilele cha maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Sherehe hizo zimefanyika katika Uwanja wa Gombani, wilaya ya Chakechake, mkoa wa Kusini Pemba.

Mgeni rasmi wa maadhimisho haya alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Katika hotuba yake, Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kuenzi Mapinduzi hayo kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, kukuza uchumi, na kuhakikisha kila Mzanzibari ananufaika na matunda ya Mapinduzi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Rais Samia amepongeza juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Mwinyi katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku akiahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Maadhimisho haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa pamoja na wananchi kutoka kila kona ya Zanzibar na Tanzania Bara. Burudani za kiutamaduni, gwaride rasmi, na maonesho ya maendeleo vilihitimisha sherehe hizi kwa mafanikio makubwa.


No comments:

Rais Samia Aungana na Watanzania Kuadhimisha Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanMhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 12 Januari, 2025, ameungana na wananchi wa Zanzibar kusherehekea ...