Monday, January 20, 2025

Rais Samia Afanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Ikulu Chamwino






Dodoma, 20 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, katika Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na WHO katika sekta ya afya, hususan kwenye maeneo ya kuboresha huduma za afya, kukabiliana na magonjwa ya mlipuko, na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya afya nchini.

Rais Samia alieleza dhamira ya serikali ya kuendelea kuwekeza katika sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, huku Dkt. Tedros akipongeza juhudi za Tanzania katika kuimarisha mifumo ya afya na kushiriki kikamilifu katika masuala ya afya kimataifa.

Mazungumzo haya yanadhihirisha ushirikiano madhubuti kati ya Tanzania na WHO, katika kuhakikisha ustawi wa afya ya Watanzania na dunia kwa ujumla.

 

No comments:

🔴🔴HIFADHI YA MPANGA-KIPENGERE YAENDELEA KUWA LULU YA VIZAZI VIJAVYO

  📍Wanafunzi wa Nyanda za Juu Kusini Wapiga Kambi Kujifunza na Kutali  Na Beatus Maganja, Njombe. Wahenga walioshiba tunu za uhifadhi na ut...