Sherehe ya hadhi ya kifalme inayojulikana kama Mati Tanzanite Royal Party imefanyika Mjini Babati Mkoani Manyara huku mamia ya wahudhuriaji wakivalia mavazi ya kifahari ya falme mbali mbali za Kiafrika na Duniani ,sherehe hizo zimezua gumzo kutokana na aina ya mavazi,chakula na burudani zilizotolewa na wanamuziki wakubwa wakiongozwa na Msanii Rayvanny.
Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited David Mulokozi ambaye pia ni muandaaji wa sherehe hizo amesema zimelenga kuwapongeza wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa .
“Kampuni ya Mati Super Brands Limited iliyoanza kama mchicha na sasa imekua mbuyu ,ilianza kama mradi mdogo wa kuhudumia mikoa michache ya Tanzania lakini leo tuna wateja nchi nzima na karibia Afrika nzima.Haya ni matokeo ya Usimamizi thabiti wa viongozi wetu” Anaeleza Mulokozi
Aidha amesema kuwa umakini na umahiri wa Wafanyakazi na Viongozi hususan idara ya uzalishaji kupitia utafiti na maendeleo kwa kutengeneza bidhaa mpya ya Tanzanite Royal Gin ambayo imeleta mapinduzi makubwa kwenye soko la vinywaji duniani.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda ameipongeza Kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kulipa kodi stahiki za serikali na kutoa fursa za ajira kwa vijana hivyo kupunguza changamoto ya ajira katika mkoa wa Manyara na Taifa.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na Watu Mashuhuri ikiwemo Msanii Rayvanny ,Mtayarishaji Mkongwe wa Bongo Fleva P.Funk Majani,Babu wa Tik Tok,Zuli Comedy,Viongozi wa Siasa na Wafanyabiashara mbali mbali.
No comments:
Post a Comment