Tuesday, January 07, 2025

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI UAPISHO WA RAIS WA GHANA MHE. JOHN MAHAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpongeza Rais wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Independence Square Jijini Accra nchini Ghana leo tarehe 07 Januari 2025.


Rais Mteule wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama akiapa kuwa Rais wa Taifa hilo katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Independence Square Jijini Accra nchini Ghana leo tarehe 07 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika zilizofanyika Uwanja wa Independence Square Jijini Accra nchini Ghana kuhudhuria uapisho wa Rais Mteule wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama leo tarehe 07 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Uapisho wa Rais Mteule wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama uliyofanyika katika Uwanja wa Independence Square Jijini Accra nchini Ghana wa tarehe 07 Januari 2025.


 Rais Mteule wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama akiapa kuwa Rais wa Taifa hilo katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Independence Square Jijini Accra nchini Ghana leo tarehe 07 Januari 2025

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ,leo tarehe 07 Januari 2025 amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za Uapisho wa Rais wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama.

Sherehe hizo za uapisho zimefanyika katika Uwanja wa Independence Square uliopo katika Jiji la Accra nchini humo. Pia Makamu wa Rais wa Ghana Mhe. Prof. Naana Jane Opoku-Agyemang ameapishwa katika sherehe hiyo.

Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika, wawakilishi wa Jumuiya na Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa Dini, Vyama vya siasa na wananchi mbalimbali.

Mara baada ya uapisho huo, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango aliwapongeza Rais wa Ghana Mhe. John Mahama pamoja na Makamu wake Mhe. Prof. Naana Jane Opoku-Agyemang.

Katika hafla hiyo, Makamu wa Rais ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Judica Nagunwa.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
07 Januari 2025
Accra – Ghana.

No comments:

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZISHI YA MWENYEKITI WA ZAMANI WA CCM LIWALE

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akishiriki katika mazishi ya Mwenyekiti wa zamani w...