Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO bado linasubiri ushirikiano kamili kutoka kwa serikali ya China ili kufafanua chanzo cha janga la UVIKO-19 pia katika salamu zake za mwaka mpya akisisitiza amani duniani.
Hii ni miaka mitano baada ya visa vya kwanza vya ugonjwa mpya wa mapafu (Uvico 19) kuripotiwa katika mji wa China wa Wuhan. WHO imesema jijini Geneva kuwa hilo ni sharti la kimaadili na kisanyasi.
Shirika hilo la Afya Ulimwenguni linaloongozwa na Mkurugenzi Mkuu wao Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus (pichani) limeitaka China kutoa data zote ili wanasayansi waelewe chimbuko la janga hilo lililotikisa dunia na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.
Taarifa ya WHO imesema kuwa bila uwazi na ushirikiano miongoni mwa nchi tofauti, dunia haiwezi kuzuia na kujiandaa vya kutosha kwa magonjwa ya milipuko na majanga ya siku za usoni.
Wakati huo huo Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa wito kwa viongozi “kuleta amani inayohitajika sana duniani, afya na usalama kwa wote,” akisisitiza kwamba “amani ni, na daima itakuwa, dawa bora kwa afya na ustawi wa watu wote, kila mahali.”
Kupitia ujumbe wake wa video wa mwishoni wa mwaka, Tedros amekumbusha kwamba wakati wa wiki ya Krismasi, alikuwa Yemen katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa kujadiliana na mamlaka ya nchi hiyo ili kuachiliwa kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wasaidizi wengine wa kibinadamu.
No comments:
Post a Comment