Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) akikabidhi tuzo maalum kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kulia) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha ujenzi Kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Wilaya ya Kusini, Unguja wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kituo hicho iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Afya Zanzibar Bw Nassor Ahmed Mazrui (Kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Kulia)
Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete
amepongeza ushirikiano baina ya wadau binafsi na serikali katika
kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ile inayohusiana na
afya, akibainisha kuwa hatua hiyo ni chachu muhimu zaidi katika
kuchochea kasi ya maendeleo nchini.
Dkt.
Kikwete alitoa pongezi hizo mwisho wa wiki wakati akizindua rasmi Kituo
cha Afya cha kisasa cha Kizimkazi kilichopo Wilaya ya Kusini, Unguja,
Zanzibar kilichojengwa kwa ushirikiano baina ya serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na wadau mbalimbali hususani Taasisi ya Samia Foundation,
Taasisi ya Ahmed Al Falas Foundation na Benki ya Taifa ya Biashara
(NBC).
Hafla fupi ya
uzinduzi wa kituo hicho chenye thamani ya sh bil 4.4 ilihudhuriwa na
wadau mbalimbali wa sekta ya afya visiwani Zanzibar akiwemo Waziri wa
Afya Zanzibar Bw Nassor Ahmed Mazrui, Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Zanzibar, Dkt Mngereza Mzee Miraji na viongozi mbalimbali waandamizi wa
chama na serikali.
Zaidi,
walikuwepo viongozi na maofisa wa taasisi hizo wadau ambapo taasisi ya
Samia Foundation iliongozwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo ambae pia ndio
Mhandisi wa mradi huo, Mhandisi Fatma Kara, Muwakilishi wa Taasisi ya
Ahmed Al Falas Foundation na maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi pamoja na wananchi.
“Ushirikiano
na ubia baina ya serikali na wadau mbalimbali ikiwemo taasisi binafsi
ni njia rahisi zaidi katika kuchochea kasi ya maendeleo kwa faida ya
wananchi. Ushirikiano wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Taasisi ya
Samia Foundation, Taasisi ya Ahmed Al Falas Foundation na Benki ya NBC
hadi kufanikisha mradi huu ni muendelezo wa mifano mizuri ya
kuigwa…hongereni sana,’’ alipongeza Dkt Kikwete.
Zaidi
Dkt Kikwete aliepata wasaa wa kutembelea na kukagua sehemu mbalimbali
za kituo hicho alitoa wito kwa viongozi wa serikali na uongozi wa kituo
hicho kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi sambamba na kutunza
miundombinu mbalimbali ya kituo hicho ili kiendelee kutoa huduma bora
inayosadifu dhamira ya kuanzishwa kwake.
“Kufuatia
uzinduzi wa kituo hiki cha kisasa zaidi, matarajio ni kwamba wagonjwa
wengi wa maeneo haya na jirani watapata huduma za afya huku pasipo kuwa
na ulazima wa kwenda hospitali nyingine mbali kidogo na hapa. Hata hivyo
ipo haja ya kuhakikisha wataalamu wote muhimu wanapatikana hapa ili
kuakisi nia njema za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia
Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Hussein
Mwinyi,’’ alisisitiza Dkt Kikwete.
Awali
wakizungumza kwenye hafla hiyo Waziri Mazrui na Katibu Mkuu Dkt
Mngereza walisema uzinduzi huo ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 61 ya
Mapinduzi ya Zanzibar na kwamba ujenzi wa kituo hicho utasaidia
kuhudumia wananchi 13,000 kutoka maeneo ya Kizimkazi Mkunguni, Kibuteni,
kizimkazi Dimbani na maeneo ya jirani ndio utatumika kama kiwango
sahihi cha ubora kitakachotumika katika ujenzi wa vituo vingine
vitakavyoendelea kujengwa visiwani Zanzibar.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Unguja na
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation, Bi Wanu Hafidh
Ameir alisema ujenzi wa kituo hicho cha afya kwa kiasi kikubwa
utasaidia kusogeza huduma za afya kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo
hususani wanawake ambao wengi wao walikuwa wanahofia kubeba ujauzito
kutoka na huduma za afya kuwa mbali na makazi yao.
“Baada
ya ujio wa kituo hiki naamini sasa wanawake wa eneo hili mtaongeza kasi
ya kuzaa kwa kuwa idadi ya watoto waozaliwa eneo hili ipo chini sana
ikilinganishwa na maeneo mengine,’’ alisema Bi Wanu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw Theobald Sabi
alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye mradi huo ni muendelezo wa
jitihada zake kupitia sera yake ya Uwajibikaji kwa Jamii (Citizenship),
ambapo benki hiyo imeeendelea kutenga sehemu ya faida yake kila mwaka
ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika sekta za afya, elimu,
mazingira, elimu ya fedha, na ajira.
“Katika
kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Benki ya NBC imetoa zaidi ya
shilingi bilioni 4 kwa jamii. Leo, tunapozindua Kituo hiki cha Afya cha
Kizimkazi, tunajivunia kuwa miongoni mwa wadau wakubwa waliofanikisha
ujenzi wa kituo hiki muhimu. Tumechangia kiasi cha shilingi milioni 400
katika ujenzi wa kituo hiki ambacho kitaleta ahueni kubwa katika
upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wakazi wa Kizimkazi na maeneo
jirani wakiwe wakina mama na watoto’’ alisema Sabi
Zaidi,
Sabi alisema benki hiyo imejipanga kuweka mfumo maalum wa malipo ya
kidijitali katika kituo hicho cha afya utakaojumuisha Mashine ya kutolea
fedha (ATM) na Mashine za malipo kwa kadi (Point of Sale – POS) ili
kuongeza ufanisi na urahisiwa malipo kwa wagonjwa na watendaji wa kituo
hicho.
Kwa upande wake
Mhandisi Kara, alisema nia ya Taasisi ya Samia Foundation ni
kuhakikisha miradi kama hiyo inatekelezwa zaidi katika maeneo mbalimbali
hapa nchini.
Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete (kushoto) pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama na serikali visiwani Zanzibar wakisikiliza taarifa fupi kuhusu Kituo kipya cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Wilaya ya Kusini, Unguja kutoka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya Samia Foundation ambae pia ndio Mhandisi wa mradi huo, Mhandisi Fatma Kara (alieshika fimbo) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kituo hicho iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kulia). Benki ya NBC ni mmoja wa wadau muhimu kwenye ujenzi wa kituo hicho kilichojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Samia Foundation.Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete (wa tatu kushoto) pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama na serikali visiwani Zanzibar wakisikiliza maelezo kuhusu vifaa tiba mbalimbali vilivyopo kwenye Kituo kipya cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Wilaya ya Kusini, Unguja kutoka kwa mmoja wa wataalam wa afya kituoni hapo (alieshika mic) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kituo hicho iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
“Ushirikiano na ubia baina ya serikali na wadau mbalimbali ikiwemo taasisi binafsi ni njia rahisi zaidi katika kuchochea kasi ya maendeleo kwa faida ya wananchi. Ushirikiano wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Taasisi ya Samia Foundation, Taasisi ya Ahmed Al Falas Foundation na Benki ya NBC hadi kufanikisha mradi huu ni muendelezo wa mifano mizuri ya kuigwa…hongereni sana,’’ - Dkt Kikwete.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya NBC, Bw Theobald Sabi (pichani) alisema ushiriki wa benki
hiyo kwenye mradi huo ni muendelezo wa jitihada zake kupitia sera yake
ya Uwajibikaji kwa Jamii (Citizenship), ambapo benki hiyo imeeendelea
kutenga sehemu ya faida yake kila mwaka ili kusaidia kutatua changamoto
mbalimbali katika sekta za afya, elimu, mazingira, elimu ya fedha, na
ajira.
No comments:
Post a Comment