Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja (kulia) mara alipowasili katika ofisi za Puma Energy jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua shughuli zake.
Meneja Afya, Usalama na Mazingira kutoka katika kampuni ya Puma Energy Blasio Menchi (kulia) akielezea shughuli za kampuni hiyo mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo pamoja na ujumbe wake.
Kutoka kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dk. Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini James Andelile, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja,na Kaimu Kamishna wa Petroli ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mwanamani Kidaya wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Afya, Usalama na Mazingira kutoka katika kampuni ya Puma Energy Blasio Menchi (hayupo pichani) kwenye ofisi za Puma Energy jijini Dar es Salaam.
Meneja Uendeshaji kutoka Kampuni ya Puma Energy Lameck Hiliyai (katikati) akielekeza jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini James Andelile (aliyekaa katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja (kulia) katika kikao hicho kwenye ofisi za Puma Energy jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini James Andelile (kulia) wakibadilishana mawazo katika kikao hicho.
No comments:
Post a Comment