Monday, June 20, 2016

MANGULA AZINDUA KITABU CHA “MAJIPU YA NCHI YETU” TUSHIRIKIANE KUYATUMBUA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akizindua Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Bi. Deborah Charles, Agusto Matefu, Mwenyekiti wa Kamati ya Mijadala na Kongamano ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na wa mwisho kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo inalengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akionyesha Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua mara baada ya kukizindua leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Amosi Siyantemi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi yetu “ Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na kushoto Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi Yetu “Tushirikiane kuyatumbua” leo jijini jijini Dar es Salaam. Kitabu hiko kimezinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula (hayupo pichani).Uzinduzi wa Kitabu hicho umeenda sambamba na utambulisho wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM). Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.

Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...