Monday, June 13, 2016

ZAIDI YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 36 ZIMETUMIKA KATIKA KUFIKISHA HUDUMA ZA MAWASILIANO YA SIMU KATIKA MAENEO YA VIJIJINI

Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard akimuonyesha ramani inayoonyesha maeneo ambayo mfuko umetekeleza miradi ya kupeleka huduma za mawasiliano baadhi ya wa wananchi waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO leo jijini Dar es Salaam.
VIJ2Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard akiwaelezea jambo baadhi ya wa  wananchi  wa Dar es salaam waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO .
VIJ3Mwanasheria wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Ambokile Mwakaje (Kulia) akimuelekeza baadhi ya maeneo walipotekeleza miradi ya huduma za mawasiliano mmoja wa mwananchi  aliyetembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO.
VIJ4Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Edwin Makala akiwaelezea jambo baadhi ya wa es Salaam wananchi waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO.
VIJ5Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard akiwaelezea jambo baadhi ya wa es Salaam wananchi waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO.
VIJ6Baadhi ya wananchi wakiwa katika banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wakati wa maonyesho ya SIMU EXPO 2016 leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija,MAELEZO
…………………………………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija,MAELEZO
Zaidi ya dola za kimarekani milioni 36 zimetumika katika kufikisha huduma za mawasiliano ya simu katika maeneo ya vijijini yasiyo na mvuto wa kibiashara nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard wakati wa maonyesho ya SIMU EXPO 2016 leo jijini Dar es Salaam.
Mfuko wa Mawasiliano kwa wote unashiriki maonyesho hayo ili kutoa elimu kwa umma juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
Albert amesema kuwa kazi kubwa ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ni kufikisha huduma za mawasiliano ya simu katika maeneo yote ya vijini yasiyo na mvuto wa kibiashara ambapo makampuni ya simu yanasuasua kupeleka huduma hiyo.
“Sisi kama Taasisi ya Serikali kazi yetu kubwa ni kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo yote ya vijini ambayo makampuni binafsi yanasuasua kupeleka huduma kutokana na msukumo wa kibiashara.” Alisema Albert.
Aliongeza kuwa mradi wa kwanza uliotekelezwa na mfuko huo umegharimu takribani Dola za Kimarekani milioni 5.8 ambapo jumla ya Kata 52 zimenufaika na mradi huu kwa kuunganishwa na huduma za mawasiliano ya simuK.
Pamoja na jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma za mawasiliano ya simu kumekuwa na changamoto katika kutekeleza azma hiyo kwa wakati kutokana na ufinyi wa bajeti na kukosekana kwa miundombinu rafiki kama vile Barabara na Umeme.
Kutokana na changamaoto hizo Albert ametoa rai kwa jamii kuwa na subira wakati utekelezaji wa miradi ya kupeleka huduma za mawasiliano ya simu katika maeneo yao ukiendela hatua kwa hatua kadri fedha zinavyopatikana.
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2006  kwa lengo la kupeleka na kufanikisha mmawasiliano kwa wananchi waishio katika maeneo machache ya mijini na maeneo mengi ya vijijini yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa watoa huduma ya mawasiliano.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...