Wednesday, June 29, 2016

MAHAKAMA KUU JIJINI ARUSHA YAMVUA UBUNGE MBUNGE WA LONGIDO ONESMO OLE NANGOLE (CHADEMA),YAAMURU UCHAGUZI URUDIWE UPYA

Aliyekwa Mbunge wa Jimbo la Longido,Mh.Onesmo Nangole

Kesi iliyokuwa ikiunguruma kuanzia  Februari 29 ,2016 katika Mahakam Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii

Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dkt Kiruswa  alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido Mh.Onesmo Nangole.

Akisoma hukumu hiyo,Jaji Mwagesi  alisema kuwa mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.Katika shauri hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni:

1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole.
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole

3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura

4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.

5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo

Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;"Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa sheria,Natamka kwamba;

Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...