Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akiwa na viongozi wa Taifa la Nigeria na Shirika la Makazi la Afrika Jijini Abuja wakati ukipigwa wimbo wa Taifa la Nigeria katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika.
………………………………………………………………………………………………………………………
Katika kutambua mchango wa Tanzania katika uendelezaji wa makazi ya watu na kuweka mbele utu wa binadamu wa mahitaji ya msingi ikiwemo nyumba, wajumbe kutoka nchi 44 za kiafrika waliohudhuria Mkutano wa 35 wa Shirika la Makazi la Afrika Jijini Abuja Nigeria, kwa pamoja wameiteua na kuiidhinisha Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa Shirika hilo utakaofanyika mwaka 2018.
Katika Mkutano Mkuu wa Abuja changamoto iliyojitokeza ni uwezo wa nchi za kiafrika wa kuwapatia wananchi wake nyumba za gharama nafuu, huku wajumbe wakitoa rai kwa serikali zao kuainisha vigezo vya kutambua nyumba ya gharama nafuu. Aidha, wajumbe wa Mkutano huo wanaona changamoto kubwa ya wananchi wengi wa Afrika kuweza kumiliki nyumba ya gharama nafuu ni uwezo mdogo unaotokana na vipato vidogo, kutokuwepo sera ya kuwezesha raia kumiliki nyumba za gharama nafuu, kukosekana kwa miundombinu katika makazi ya gharama nafuu, riba kubwa za mikopo ya ujenzi wa nyumba nafuu na ukosefu wa ardhi ya kujenga nyumba hizo.
Kwa ujumla changamoto za nchi za kiafrika katika kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana na kilio kikubwa katika nchi hizo ni kuwepo makazi holela hata baada ya nchi hizo kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe. Hivyo, Mkutano Mkuu huu umeazimia nchi wanachama kuweka juhudi katika kuipa kipaumbele sekta ya nyumba kwa kuwa ni sekta mtambuka katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na maisha bora ya watu.(Habari za mkutano huo katika picha na Muungano Saguya, Abuja, Nigeria)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula (wan ne kulia) akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique). Wengine ni Waziri wa Nishati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde Fashiola (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shelter Afrique Bw. James Mugerwa (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shelter Afrique Bw. Jean-Paul Missi (wa kwanza kulia).
Mkurugenzi Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje (wa pili kushoto) akiwa miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique uliofanyika Jijini Abuja wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje (wa pili kushoto) akiwa miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique uliofanyika Jijini Abuja wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akiwa meza kuu baada ya Tanzania kuteuliwa na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique Jijini Abuja kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 37 utakaofanyika nchini Tanzania mwaka 2018.Kulia kwa Naibu Waziri ni Waziri wa NIshati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde Raji Fashola ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Wajumbe kutoka nchi 44 za Afrika na wageni waalikwa kutoka nchi na mashirika mbalimbali ya Kimataifa wakiendelea na Mkutano wa 35 wa Shirika la Makazi la Afrika uliofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton Jijini Abuja, Nigeria. Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akiwa katika kilima cha Katampe Jijini Abuja, ambacho ni katikati ya nchi ya Nigeria alipotembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique). Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akiwa katika kilima cha Katampe Jijini Abuja, ambacho ni katikati ya nchi ya Nigeria alipotembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique). Kutokana na hali ya amani katika nchi hiyo, Naibu Waziri alipata ulinzi wa kutosha kama inavyoonekana alipopiga picha ya pamoja na walinzi walioandamana na wageni kutoka nchi mbalimbali katika ziara hiyo. Tudumishe amani yetu Tanzania
Mchoro huu juu na chini unaonyesha taswira ya mji wa kisasa unaotabiriwa kuwa Dubai ya Nigeria unaojengwa nje kidogo ya Jiji la Abuja ujulikanao kama Centenary City Abuja ambao wajumbe wa nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika waliweza kuutembelea na kujionea ndoto ambayo wanigeria wameamua kuitekeleza.
No comments:
Post a Comment