Friday, June 24, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AKUTANA NA WAZIRI KUTOKA MALAYSIA NA MAKAMU WA RAIS WA TIGO AFRIKA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala (kushoto) mara baada ya mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji
Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais wa Tigo Afrika Bi. Rachel Samren (Kushoto) wakati Bi. Rachel Samren alipomtembelea Makamu wa Rais  ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Juni 2016.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa Tigo Afrika Bi. Rachel Samren wengine pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kisheria Bi. Sylvia Balwire na Bi. Halima Okash Afisa Uhusiano (wa kwanza kushoto)  Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Juni 2016.
——————————————————–
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameiomba serikali ya MALAYSIA kujenga ofisi za ubalozi wake hapa
nchini ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. 
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo Juni 24, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA ambaye
aliongozana na Balozi wa MALAYSIA aliye na makazi yake jijini Nairobi Kenya, ISMAIL SALAM walipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar Salaam.
Makamu wa Rais amesema ujenzi wa ofisi za ubalozi huo hapa nchini utarahisisha kwa kiasi kikubwa Watanzania wanaotaka kusafiri kwenda nchini
MALAYASIA kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za masomo na biashara kuliko hali ilivyo sasa ambapo ofisi za balozi hizo zipo Nairobi – Nchini KENYA.
Kwa upande wake Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi yake itaendelea kuimarisha,kukuza
na kuendeleza mahusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia hasa uanzishaji wa ubalozi wake hapa nchini.
Hata hivyo, Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa Makubaliano ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia ambayo
yatajikita  katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, uchukuzi na biashara.
Wakati huo huo, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN pia amekutana Makamu wa Rais wa TIGO – Afrika RACHEL SAMREN ambapo wamezungumzia masuala
mbalimbali ikiwemo namna kampuni hiyo itakavyosadia katika kuwawezesha wanawake kuondokana na umaskini hapa nchini.
Katika kuhakikisha taifa linaongeza ukusanyaji wa mapato,
Makamu wa Rais ameuhimiza uongozi wa kampuni ya Simu ya Tigo hapa nchini kuhakikisha
unalipa kodi kwa uwazi ili fedha hizo ziweze kusaidia serikali katika kuimarisha
utoaji wa huduma za kijamii hapa nchini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...