Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kushoto) akiongozana na mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakati alipofika kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam jana Juni 17, 2016 kwa ajili ya kumwakilisha Mufti Mkuu wa Tanzania katika Hafla ya Futari
iliyoandaliwa na Mfuko huo. Picha na Mafoto Blog
iliyoandaliwa na Mfuko huo. Picha na Mafoto Blog
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (katikati) mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakiwaongoza wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, kuchukua Futari wakati wa hafla Futari iliyoandaliwa na Mfuko huo katika Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam jana Juni 17, 2016.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla
hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 18, 2016. Kushoto ni mgeni rasmi, Sheikh Ali Hamis.
Mgeni rasmi Sheikh Ali Hamis, akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF,(hawapopichani) wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 17, 2016. Katikati ni Mkurugenzi mkuu wa Mfuko huo, William Erio.
*********************************************
Hivyo ameuomba uongozi wa mfuko huo uendelee na jitihada za kuwafikia wananchi kwenye maeneo mbalimbali hapa nchi na hasa maeneo ya vijijini.
*********************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
JAMII imetakiwa kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwani mfuko huo ni faraja kwa Watanzania na unaofanya mambo makubwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi.
Wito huo umetolewa na mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Ali Hamis wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na uongozi wa mfuko huo kwa wafanyakazi wake.
Alisema kuna faida kubwa kwa wananchi kujiunga na mfuko huo kwani watafaidika na mafao mbalimbali yanayotolewa na PPF. Aidha Sheikh Hamis alisema kuwa ipo haja kwa watendaji wa mfuko huo kuendelea kuwaelimisha wananchi ili waendelee kujiunga na PPF.
Alifurahishwa na namna uongozi wa mfuko huo ulivyoandaa hafla ya futari hiyo maalum kwa kuwafuturisha wafanyakazi wake na kwamba hilo ni jambo jema kwani wafanyakazi wanafahamiana na kubadilishana mawazo.
Sheikh Hamis aliitaka jamii kuwaenzi waasisi wa taifa hili kwa kuendelea kudumisha Amani na umoja kwani wamefanya jambo jema la kuwafanya wananchi wote kuwa kitu kimoja bila kujali dini wala kabila.
Kwa mujibu wa Sheikh Hamis, PPF ni aina ya mfuko unaowawezesha wananchi kujikomboa.
Hivyo ameuomba uongozi wa mfuko huo uendelee na jitihada za kuwafikia wananchi kwenye maeneo mbalimbali hapa nchi na hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa PPF, William Erio aliwashukuru wafanyakazi kwa kushiriki futari hiyo,ambayo imekuwa ikiandaliwa kika mwaka na kuwashirikisha wafanyakazi wake wote. Naye mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TUICO aliushukuru uongozi wa mfuko huo kwa kuwaandalia futari hiyo.
Futari hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa PPF kutoka makao
makuu, kanda za Ilala, Temeke na Kinondoni.
makuu, kanda za Ilala, Temeke na Kinondoni.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, Tawi la Tuico, akiwashukuru wafanyakazi wa mfuko huo kwa kushiriki kikamilifu katika hafla hiyo.
Sheikh Mohamed Ali, kutoka Baraza Kuu la Waislam Tanzania
BAKWATA, akiomba dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.
BAKWATA, akiomba dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment