Wednesday, June 22, 2016

UHURU FM YATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI VYA SH. MILIONI 3 KWA CHUO CHA UFUNDI STADI KWA WENYE ULEMAVU CHA YOMBO, DAR ES SALAAM


Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, Angel Akilimali akijaribu kushona wakati yeye na wafanyakazi wa Radio hiyo, walipowasili kwenye Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kwa wenye ulemavu kilichopo Yombo Kata ya Kiwalani Temeke Dar es Salaam, kutoa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo ni pamoja na Mchele, unga, saruji, sabuni kasha la huduma ya kwanza, mifagio, mafuta ya kula, kofia maalum kwa wenye ulemavu wa ngozi, miwani, viti, mafuta maalum kwa wenye ulemavu wa ngozi, vifaa vya michezo ambavyo ni jezi za mpira wa miguu na netiboli, mipira ya kawaida na mipira ya kengere kwa wenye ulemavu wa macho, Kamba ya kuvuta kwa ajili ya walemavu, vyote vyenye thamani za zaidi ya sh. milioni 3. zifuatazo ni picha mbalimbali kuhusiana na tukio hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, Angel Akilimali akimvalisha miwani malum, mwanafunzi wa Chuo hicho mwenye ulemavu wa ngozi.
MKurugenzi Mtendaji wa Uhuru DM Angel Akilimali akimvisha mtandio maalum mwanafuzni wa Chuo hicho mwenye ulemavu wa ngozi. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi kwa wenye ulemavu Yombo, Mariam Chellangwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM akikabidhi mpira wenye kengere ndani, kwa ammoja wa wanacfunzi wa Chuo hicho mwenye ulemavu wa macho.
Baadhi ya viongozi wa Uhuru FM, wakiwa na Mwalimu wa Chuo hicho, Aloyce Mkuna (wapili kushoto), baada ya kuwasili kwenye chuo hicho. Kulia ni Mhariri wa Habari Pius Ntiga, Meneja Rasilimali watu na Utawala Narsis Mbise, Sigoli Paul ambaye ni Mwandishi na Mtangazi
Makamu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi kwa wenye ulemavu Yombo, Mariam Chellangwa akiwakaribisha rasmi msafara mzima wa Uhuru FM ulipowasili katika chuo hicho.

Wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa katika picha za pamoja na wanafunzi wa Chuo hicho, mwishoni mwa ziara hiyo. Picha na Emmanuel Ndege. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...