Monday, June 20, 2016

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MADAWATI 50 SHULE YA MSINGI MAKOLE DODOMA


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi,Vijana na Ajira, Antony  Mavunde (kushoto), akipokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 6 kutoka kwa Mkurungenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamisi yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya Shule ya Msingi Makole iliyopo Manispaa ya Dodoma,mwishoni mwa wiki
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde (wa pili kushoto), akifurahi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makole iliypo manispaa ya Dododma mara baada ya makabidhiano ya msaada wa madawati 50 uliotolewa na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Dk. Jasmin Tsekwa (wa pilikulia) na kulia ni Mkurungenzi Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamisi. 
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma wakiwa wamekaa kwenye madawati ambayo waliikabidhi shule ya msingi makole iliyomjini Dodonma jana ,msaada huo unathamani ya zaidi ya sh milioni 6.
Mkurungenzi Benki ya CRDB tawi la Dodoma Rehema Hamisi (kulia) akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makole iliyopo mjini Dodoma, baada ya kuwakabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na wafanyakazi wa wa benki hiyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali kupunguza tatizo la madawati mashuleni.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, tawi la Dodoma, Rehema Hamisi akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa ajili ya Shule ya Msingi ya Makole Manispaa ya Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi,Vijana na Ajira, Antony  Mavunde akioa hotuba yake wakati wa hafla ya kupokea madawati 50 yaliyotolewa kama msaada na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma kwa ajili ya Shule ya Msingi Makole. 
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Makole Dodoma.
Wanafunzi wakitumbuiza kwa kuimba kwaya.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...