Tarehe 8 Juni ni siku ya Bahari Duniani. Nipe Fagio itaadhimisha siku hii kupitia shughuli mbalimbali za kuelimisha na uhamashishaji ikiwemo kampeni katika mitandao ya kijamii pamoja na michezo ya kuigiza kwenye jukwaa la wazi, katika jitihada za kutafuta ushirikiano wa umma katika swala la kuweka bahari zetu safi, hivyo basi zenye afya. Taka katika bahari inazidi kuwa miongoni mwa vitisho vikubwa kwa dunia yetu.
Watafiti waliobobea katika tafiti za bahari wametoa ripoti kuwa asilimia 40 ya sakafu ya bahari yetu imefunikwa kwa vipande vidogo vidogo vya plastiki vinavyoelea pamoja na taka nyingine. Hii inaleta madhara makubwa sio tu kwa viumbe vya bahari bali pia kwa afya zetu wenyewe, mienendo na usalama wa maisha yetu. Kwa masikitiko, maji ya bahari jijini Dar es Salaam pia yana hadithi yake.
Shughuli za kawaida kama kuogolea katika bahari au kula samaki, ambazo hapo awali zilichukuliwa kama vigezo vya mwenendo wa maisha yenye afya sasa hivi vimegubikwa na utata. Kutokana na ongezeko la ukuaji wa miji pamoja na hali duni iliyopo ya usafi na ukosefu wa huduma ya uzoaji taka, sehemu kubwa ya taka kutoka mijini inaibuka katika hali ya uchafuzi wa mazingira kwenye maeneo yasiyo rasmi kinyume cha sheria kama mito na mifereji ambayo huelekea moja kwa moja baharini.
Bila shaka, jambo hili linaleta madhara makubwa sana kwa afya ya umma na mazingira yetu. Plastiki haswa,ndiyo inayochukuwa mamia ya miaka kuoza, na inazidi kuwa mojawapo ya taka zenye utata katika mikondo yetu ya maji. Wanyama wa baharini huishia kula plastiki hizi wakifikiri ni chakula. Hii inaleta madhara makubwa kwa usalama wa viumbe vya baharini, lakini watafiti pia wanahofia afya za binadamu wanaotegemea samaki kama chanzo kikuu cha mlo wao.
Nipe Fagio, shirikisho la kijamii linalojikita katika kuboresha usafi, afya na usalama wa jiji, lilikusanya kilo 2,515 za taka katika siku moja tu ya usafi, maeneo ya Coco Beach Septemba iliyopita. Taka iliyokusanywa kwa wingi zaidi ni vizibo vya chupa, mifuko ya kufungia chakula, viatu na mifuko ya plastiki.
Nipe Fagio kwa mara nyingine inaomba ushirikiano wa umma katika kampeni ya Siku ya Bahari Duniani ambayo itakuwa na shughuli zifuatazo: Mchezo wa kuigiza katika jukwaa la wazi Coco Beach, siku ya Jumapili tarehe 12 Juni, saa kumi hadi kumi na moja jioni. Kiingilio ni bure Better Bag Challenge (Nani Mwenye Mfuko Bora), itahamasisha kukataa kutumia mifuko ya plastiki na badala yake kutumia mifuko ambayo itaweza kutumika tena na tena. #SelfiefortheSea (# Pichakwaajiliyabahari), Umma unahamsishwa kutuma picha zao zikiambatanishwa na ujumbe wenye ahadi yake kusaidia juhudi za kuweka bahari yetu safi na yenye afya.
No comments:
Post a Comment