Thursday, June 16, 2016

BODI YA WAKURUGENZI NHC YAMKABIDHI CHATI CHA UTAMBUZI ETHELDREDER KOPPA, MSHINDI WA TUZO YA MWANAMKE MGUNDUZI KIJANA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Zakhia Meghji akimkabidhi cheti cha kutambua mchango mkubwa na ushindi wa Tuzo ya Mwanamke Mgunduzi bora kijana wa chini ya umri wa miaka 30 katika sekta ya ujenzi, Etheldreder Koppa, ambaye pia ni Meneja Miradi Msaidizi wa NHC aliyekabidhiwa cheti cha ushindi kwenye tukio lilifanyika kwenye tafrija mchapalo ya jioni siku ya Jumanne (Mei 10, 2016 likiwa katika ukumbi mmoja na maonyesho ya sekta ya ujenzi ya Afrika kwenye ukumbi wa kimataifa wa Gallagher Convention Centre, Johannesburg, Afrika Kusini. Tuzo hizo za sekta ya ujenzi huibua vipaji bora na haba vya wanawake katika ujenzi wa nyumba na sekta nzima ya ujenzi na kutambua umuhimu wa wanawake katika sekta ya ujenzi. Cheti hicho cha kutambua ushindi wake kimetolewa na Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Zakhia Meghji katika picha ya pamoja na Mshindi wa Tuzo ya Mwanamke Mgunduzi bora kijana wa chini ya umri wa miaka 30 katika sekta ya ujenzi, Etheldreder Koppa na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba lamTaifa, Felix Maagi, shughuli ya utoaji cheti nilifanyika muda mfupi kabla ya kikao cha Bodi.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa Tuzo ya Mwanamke Mgunduzi bora kijana wa chini ya umri wa miaka 30 katika sekta ya ujenzi, Etheldreder Koppa.

 Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akimpongeza Mshindi wa Tuzo ya Mwanamke Mgunduzi bora kijana wa chini ya umri wa miaka 30 katika sekta ya ujenzi, Etheldreder Koppa na  shughuli ya utoaji cheti nilifanyika muda mfupi kabla ya kikao cha Bodi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...