Wednesday, June 29, 2016

MKUFUNZI WA MASWALA YA BIASHARA NA MASOKO REHEMA KASULE AWAPA ELIMU MANJANO DREAM MAKERS

Mkufunzi wa maswala ya biashara Mama Rehema Kasule kutoka nchini Uganda akiwapa elimu wanafunzi wa Manjano Foundation jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwenye majukumu yao ya kila siku ikiwemo kutengeneza uhusiano na watu waliofanikiwa kwa kuwa itasaidia kujifunza mengi.Pia namna ya kujiamini kuwaza mafanikio zaidi kuwa lazima wafanikiwe na kuachana kabisa na mawazo ya kushindwa akiwa sambamba na Afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions, Mama Shekha Nasser. 
Akieleza zaidi Mama Kasule amewataka Washiriki wa Manjano Dream Makers kama wanataka kufanikiwa kazi zao za upambaji na biashara zao ni lazima wafanye kwa moyo mmoja kutoka ndani ya nafsi pia kuachana na fikra za kukata tamaa na maneno ya watu ya kuwakatisha tamaa. Kwa upande afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na Mkurugenzi wa Manjano Foundation mama Shekha Nasser amewataka washiriki hao kuongeza juhudi pia kuyatekeleza kwa vitendo yale yote waliofundishwa katika mafunzo hayo.

Mama Rehmah Kasule alikuwa jijini Dar akihudhuria kwenye semina ya siku 4 ya #PSIPSE "Partnership to Strengthen Innovation and Practices in Secondary Education.
Baada ya semina yake, mama Kasule akajitolea siku moja kuja kutoa mafunzo kwa washiriki wa Manjano Dream Makers ikiwa ni mojawapo ya mkakati wa washiriki walio wengi wa Vital Voices (na yeye akiwa mmojawapo) kwamba kila mwanamke ajitolee kuwasaidia au kuwafundisha wanawake vijana kitu anachokijua, yaani "Pay it Forward."

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...