Pilikapilika za maandalizi ya Maonyesho ya Nane Nane kitaifa mwaka huu zimepamba moto ambapo Mgeni Rasmi katika maonesho hayo yatakayofunguliwa Jumatatu Agosti 3, 2015 anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda. Maonesho hayo ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”
Mratibu wa Maonyesho ya Nane Nane kutoka wilaya ya Newala Ado Kiwangu akiwaonesha na kuwaeleza wageni waliotembelea bustani ya michungwa juu ya namna bora ya kuzalisha machungwa ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbolea ya samadi inayoipa michungwa virutubishi stahiki, hivyo michungwa huzaa sana.
Mfugaji wa sungura Ahmed Juma Ntava akiwalisha sungura wakati wa maandalizi ya Maonyesho ya Nane Nane kitaifa mkoani Lindi mwaka huu ambapo Mgeni Rasmi katika maonesho hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda yatakayofunguliwa Jumatatu Agosti 3, 2015.
Mmoja wa watumishi wa Jeshi la Magereza nchini akivuna kabichi iliyokomaa tayari kwa matumizi ya mboga. Continue reading →
No comments:
Post a Comment