Monday, February 02, 2015

MKURUGENZI MKUU WA NHC BW. NEHEMIA MCHECHU ATEMBELEA MIRADI GEITA NA MWANZA

Msimamizi wa mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Bombambili Geita Bw, Julius Ntoga (kulia) akitoa maelezo ya mradi huo kwa ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu alipotembelea mradi huo jana. Mradi huo wenye nyumba 48 ni wa nyumba za kuuza na unakamilika Februari mwaka huu.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ukitembelea nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa eneo la Bombambili, Geita kwa ajili ya kuuzia
wananchi.
Sehemu ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo
la Bombambili Mkoani Geita
Sehemu ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo
la Bombambili Mkoani Geita
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa ufafanuzi
kwa jopo la wasimamizi wa miradi ya Shirika na watendaji wengine ya namna
wanavyoweza kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba ili wananchi wengi wa kipato
cha kati na chini waweze kumudu kuzinunua.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiwapa mawaidha
ya namna ya kupanua uwezo wa kikundi cha Vijana Kazi Wilayani Misungwi
alipokitembelea jana. Kikundi hiki ni mojawapo ya vikundi vilivyopewa na NHC
msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana ili kujiajiri. Bw.
Mchechu ameziasa Halmashauri zote nchini kusaidia makundi ya vijana kwa kuwapa
maeneo ya kufanyia kazi zao za kufyatua matofali na kuwapa tenda za ujenzi
zinazokuwepo katika Halmashauri hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akionyeshwa na
Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Misungwi eneo lililotengwa na Halmashauri hiyo
kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za gharama nafuu
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ukionyeshwa ramani yenye
eneo lililotengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana na Afisa Mipango Miji
Bw. Maduhuna Bw. Ardhi Bw. Salvatory ili NHC iweze kujenga mji
unaojitegemea(satellite town) na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Jiji la Mwanza
linalopakana na nchi za maziwa makuu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiwashauri
viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana kuona uwezekano wa kupunguza
gharama ya NHC kulipa fidia ya eneo lililotengwa kujenga mji wa kisasa. Bw.
Mchechu aliwataka viongozi hao kuitizama NHC kama chombo cha Serikali
kinachowaletea maendeleo yao na si kama mwekezaji ili kufanya upangaji wa eneo
hilo muhimu kufanyika.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ukipokelewa katika mradi wa
ujenzi wa nyumba eneo la Buswelu na Mkandarasi wa mradi huo Bw. Said Kiure(kulia)’
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu ukipewa
maelezo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na Mkandarasi wa mradi
huo Injinia Saidi Kiure walipotembelea mradi huo Jijini Mwanza jana. Suala la
kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba hizo ili ziwe nafuu lilisisitizwa na
Mkurugenzi Mkuu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiendelea
kutembezwa na Meneja wa NHC Mkoa wa Mwanza Bw. Benedict Kilimba katika mradi wa
nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Buswelu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu na ujumbe wake wakitembelea
nyumba za NHC zilizoko barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza ambazo zitaendelezwa
ili kuongeza mapato ya Shirika na taswira ya Jiji hilo.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...