Mkurugenzi wa Lino Agency ambaye ni mmoja kati ya waandaaaji wa Miss Tanznia, Hashim Lundenga
Serikali imelifungia shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana na sababu mbalimbali na ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea, ikiwemo udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye shidano hilo.
Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano hilo.
“Baada ya kupitia maelezo yote na taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni vyema tulisimamishe kwa muda ili mwandaaji ajipange upya, atakaporejea arejee kwa nguvu na kuandaa shindano lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo hivi sasa'' alisema Mngereza.
Shindano hilo limekumbwa na kashfa mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo ya kuvisha mataji warembo wasiokidhi vigezo.
Chanzo cha Habari: Gazeti la Mtanzania, December 25.
No comments:
Post a Comment