Friday, December 26, 2014

NHC yakabiliana na tatizo la moyo nchini kwa kusaidia matibabu ya watoto 53 nchini India


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
  Rais wa Lions (Host) Club ya Dar es Salaam, Mathew Levi, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Beji ya miaka 50 ya Lions Club na Makamu wa Gavana wa Club hiyo, kwa nchi za Tanzania na Uganda, Hyderali Gangji, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo wanaokwenda nchini India kutibiwa. Hafla hiyo ilifanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na 
Makamu wa Gavana wa Club hiyo, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.  

Dk Rajni Kanabar ambaye ndiye mratibu wa safari hiyo ya India na Mwenyekiti wa Regency Medical Center akizungumza kwenye hafla hiyo fupi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.

   Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.

 Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Hahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Amina Yahya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua glasi juu kumtakia heri Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya hafla fupi ya kuwaaga watoto hao. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya hafla fupi ya kuwaaga watoto hao. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya hafla fupi ya kuwaaga watoto hao. 

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limechangia kiasi cha takribani shilingi milioni 29 katika kuokoa maisha ya watoto wenye maradhi mbalimbali ya moyo nchini ambao wanaondoka leo kwenda India kwa upasuaji. Watoto hao 53 wameagwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal.

Akizungumza na wazazi wa watoto hao waliofika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Dk Bilal alililipongeza Shirika la Nyumba la Taifa pamoja na wadau mbalimbali waliojitolea kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la moyo ambalo linaongezeka kwa kasi.

"Kama Serikali hatuwezi kukabiliana na tatizo hili peke yetu hivyo nawapongeza wadau mbalimbali binafsi na taasisi zilizojitolea kwaaajili ya kuokoa maisha ya Watanzania wenzao, ni jambo linalotia faraja na ni desturi ya Watanzania kusaidiana,"alisema.

Alisema Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kujenga taasisi za kukabiliana na tatizo hilo nchini ili kusudi hudma ziweze kuwafikia Watandania wengi zaidi.

Naye Mratibu wa magonjwa ya moyo katika Klabu ya Lions ya Dar es Salaam, Dk. Rajni Kanabar, alisema wagonjwa hao watatibiwa katika hospitali mbalimbali nchini India.

Alisema safari ya wagonjwa hao imeratibiwa kwa pamoja na Klabu ya Lions ya Dar-es-Salaam (Host), Regency Medical Centre na Wizara ya Afya ya Zanzibar.
Alisema katika kundi hilo, watakuwamo wauguzi wawili na madaktari wawili na wanatarajiwa kurudi nyumbani baada ya wiki nne zijazo.

Dk. Kanabar alisema wagonjwa 15 watatibiwa katika hospitali ya Jaypee Health Care Heart Institute iliyoko mji wa New Delhi na wengine 27 watatibiwa katika taasisi kubwa ya Fortis Escorts Heart iliyoko New Delhi, India.

"Watafanyiwa upasuaji ambao utagharimu Dola 2,500  za Marekani kwa kila mgonjwa na watapewa Dola  500 kwa ajili ya kujikimu wakiwa huko," alisema Dk. Kanabar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Medical Centre.

Alisema hospitali ya  Escorts ni miongoni mwa hospitali kubwa duniani kwa matibabu ya moyo na imekuwa ikiwafanyia upasuaji wagonjwa wa moyo kutoka Tanzania kwa punguzo kubwa la gharama za matibabu hayo.

Aliishukuru Wizara ya Afya ya Zanzibar kwa kuchangia nauli za ndege kwa wagonjwa 33 na kutoa Dola 500 kwa kila mgonjwa na Ubalozi wa India ambao viza za bure kwa wagonjwa wote kupitia balozi wa nchi hiyo hapa nchini, Debnath Shaw.

Dk. Kanabar aliwataja wengine waliochangia kuwa ni Bank M  iliyochangia Dola 10,000 gharama za upasuaji wa wagonjwa wanne, Shirika la Nyumba la Taifa limechangia shilingi milioni 29
na Klabu ya Lions Dar es Salaam (Host) Dola 16,500,  Pradeep Kumar wa Bengaluru, India Dola 16,400,  Regency Medical Centre Dola 12,500, wanafunzi wa British Columbia University Vancouver, Canada na Jumuiya ya  Theosophical ya Dar es Salaam Dola 10,000.

Wengine ni Riyaz Hassan Ali wa Karim Foundation Marekani Dola 9,000, Familia ya Mohamed Gulam Dewji Dola 5,000, Africarriers Dola 5,000, Lakhan Pal wa Dar es Salaam Dola 2,500, Nashrin Sarkai wa Marekani Dola 5,000, Hazi Abbas wa Dar es Salaam Dola 2,500, Lion Siraz Jessa wa Dar es Salaam Dola 2,500,  Lion Mohamed Laljee, Lion Yusuf Dalal, Lion Karim Meetha, Lion Nazmu Dola 3,500, Guru Sikh Sabha wa Dar es Salaam Dola 5,000, Harun Zacharia, Salim Turkey Dola 5,000, Dk. Kiran Nad Pallavi Patel wa Global Foundation Marekani Dola 10,000, Habib African Bank ya Dar es Salaam Dola 3,000 na Prem Kapoor & Family ya Mwanza Dola 3,000 na Gavana wa District 411B.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...