Wednesday, December 17, 2014

WAWAKILISHI WA MABARAZA YA WAZEE WA KIMILA WAKIMASAI WAKUTANA NA KINANA

  •  Wazee wa Kimasai wamuhakikishia Kinana uaminifu wao kwa CCM
  • Wataka wafugaji wamilikishwe ardhi
  • Waitaka serikali kuboresha maisha ya wafugaji
  • Wataka wazawa wapewe kipaumbele zaidi
  • Watoa salaam kwa Rais ,wampa pole na wamshukuru kwa kutimiza ahadi yake ya kuwapa mifugo.
 Diwani wa Viti Maalum Ngorongoro Tina Timan akizungumza wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alitaka mamlaka husika kubadili sheria kandamizi ili jamii ya Wamasai wafaidike na ardhi yao .
 Mwakilishi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Diwani Viti Maalum Maanda Mgoitiko akichangia mada wakati wa mkutano wa Wawakilishi wa Mabaraza ya Wazee wa Kimila wa Kimasai na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Mzee wa Kimila kutoka Ngorongoro Jerubi Mkati akizungumza wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Lembulung Ole Kosyando kutoka Kiteto akizungumza juu ya migogoro ya ardhi inayowakabili ambapo alisema viongozi wa kiserikali na wa kisiasa wanamiliki ardhi kubwa kinyume na taratibu kiasi cha kuleta migongano mikubwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza kwa makini pamoja na Mbunge wa Longido Ndugu Michael Lekule Laizer (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole.
 Sarah Yohana akizungumzia namna wanawake wa Kiteto wanavyoishi kwa mashaka kutokana na maisha yao kuwa hatarini na kuitaka serikali kufanya juhudi katika kutatua migogoro iliyokithiri Kiteto.
Doroh M. Kipuyo Diwani wa Monduli (Wanawake) akizungumzia jinsi wamasai wanavyoumia kuona Serikali haichukui hatua za haraka kwenye matatizo yanayowakabili.
 Wazee wa Kimila wa Kimasai wakiandika yale muhimu wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika Namanga.
 Leboi Sumuni kutoka Monduli akielezea namna wamasai walivyo na mapenzi na Chama Cha Mapinduzi na kutaka Chama hicho kionyeshe mapenzi kwa wamasai kwa kusaidia kutatua kero zao ambazo zinaonekana kuwa kubwa siku hadi siku.
 Wazee wa Kimila wakifuatilia mkutano.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana( kulia) akisikiliza kwa makini wazee wa kimila wa Kimasai pamoja na Mbunge wa jimbo la Longido Michael Lekule Laizer ambaye alisaidia kutafsiri baadhi ya hoja zilizozungumzwa kwa lugha ya kimasai.
 Philipo Kiloe Laiser Diwani wa kata ya Lubomba Longido akizungumzia Wazee wa Kimasai na kuwaelezea kuwa ni watu wenye hekima busara na wanatambulika kwenye jamii.
Esupat Ngulupa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido akichangia jambo wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mzee wa Kimila wa Kimasai wakifuatilia kwa makini mkutano huo ambao ni hatua zaidi za kutafuta suluhisho la migogoro yao .
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole. akiongea machache kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu kuongea.
 Mbunge wa Longido Michael Lekule Laizer akizungumzia masuala mbali mbali yanayoikabili  jamii ya kimasai na namna ya kuyatatu ikiwa pamoja na kujengwa kwa viwanda vitakavyodhalisha bidhaa zitokanazo na mifugo.
 Mbunge wa Kiteto Benedicto Ole Nangole akizungumza wakati wa kikao hicho.
 Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka akichangia mada wakati wa mkutano wa Wazee wa Kimila wa Kimasai na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alisema suala zima la ajira liwe kwenye uwiano wa sura ya nchi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wazee wa Kimila wa Kimasai na kuahidi kuyafanyia kazi matatizo yanayowakabili kwa muda mrefu kwa kushirikiana na wabunge wa CCM
 Viongozi wakimila wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe la baraza la Wazee wa Kimila mara baada ya kumaliza mkutano.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...