Friday, December 12, 2014

MBATIA AWANADI WAGOMBEA WA CHAMA NCCR-MAGEUZI KATIKA JIMBO LA VUNJO


Kikundi cha Nyimbo cha Mlimbo Uwo kikitoa burudani wakati wa kampeni za Chama cha NCCR-Mageuzi za kuwanandi wagombea wa nafasi mbalimbali katika kijiji cha Mlimbo Uwo katika jimbo la Vunjo.

Wananchi katika kijiji cha Mlimbo Uwo wakijibu salamu ya chama cha NCCR-Mageuzi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Mlimbo Uwo. 
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi,James Mbatia akimtambulisha mwenyekiti wa kitongoji cha Pangara ,Humphrey Machange aliyepita bila kupingwa katika kitongoji hicho kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia akihutubia wananchi katika kijiji cha Mlimbo Uwo wakati akiwanadi wagombea katika kampeni za kuwania nafasi mbalimbali za ungozi katika kijiji hicho.
Diwani wa kata ya Mwika Kusini kwa tiketi ya TLP,Meja Jesse Makundi akizungumza katika mkutano wa kampeni wa kuwanadi wagombea wa chama cha NCCR-Mageuzi katika kijiji cha Mlimbo Uwo.
Diwani wa kata ya Kilema Kusini kupitia TLP akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia wakati wa mkutano wa kampeni za kuwanadi wagombea wa nafasi za Uenyekiti katika kijiji cha Mlimbo Uwo.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akionesha kitabu alichoandika kuhusu Uwajibikaji katika Uongozi ,kitabu ambacho amekigawa jimbo zima la Vunjo.
Wananchi katika kijiji cha Maring'a wakimpokea Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia kwa majani ya Masale wakati alipofika kuwanadi wagombea wa nafasi za Uenyekiti kupitia chama hicho.
Diwani wa kata ya Miwka Kusini kwa tiketi ya TLP ,Meja Jesse Makundi akihutubia katika mkutano wa kampeni wa chama cha NCCR-Mageuzi akiwanadi wagombea wa chama hicho katika kijiji cha Maring'a.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akiwahutubia wananchio katika kijiji cha Maring'a katika jimbo la Vunjo.
Wananchi katika kijiji cha Maring'a wakimshangilia mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi wakati alipohutubia katika mkutano wa hadhara katika kijiji hicho.
Mh Mbatia akimnadi mgombea wa nafasi ya uenyekiti katika kijiji cha Maring'a.
Wagombea wa nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri wakiwa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi wakati wa mkutano wa kuwanadi wagombea wa chama hicho uliofanyika katika kijiji cha Maring'a.
Mh,Mbatia akitoka katika uwanja wa ofisi za kijiji cha Maring'a mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni katika kijiji hicho.
Mh Mbatia akipokewa na wakazi wa kijiji cha Lole alipofika kwa ajili ya kuwanandi wagombea wa nafasi auenyekiti katika kijiji hicho
Mh Mbatia akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lole katika jimbo la Vunjo.
Wananchi katika Jimbo la Vunjo wakiwa wamembeba ,Mwenyekiti wa taifa wa chama cha NCCR-Mageuzi ,James Mbatia aliyefika jimbooni humo na kufanya mikutano katika vijiji mbalimbali kuwanadi wagombea wa chama hicho na wale wanaotokana na UKAWA 


Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya kaskazini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...