Kocha Van Der Pruijm akiwa na Shaffih Dauda mara tu baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere
Kocha wa zamani wa Yanga mdachi Hans Van Der Pruijm amesema amerudi tena kwenye timu yake ya zamani kuendeleza pale alipoishia,
‘Falsafa yangu ipo pale pale ya kucheza soka la kushambulia, kwasababu naamini ili ushinde mchezo ni lazima ufunge mabao ya kutosha’.
Van Der Pruijm akifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Clouds TV mara tu baada ya kutua usiku wa saa nane na nusu usiku.
Kocha huyo amesema bado hajasaini mkataba ila ana matumaini makubwa atamalizana na wakurugenzi wa klabu pale watakapokutana,
Van Pruijm anakuja kuziba pengo la kocha aliyetimuliwa Mbrazil Marcio Maximo . SOURCE
No comments:
Post a Comment