Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake jana jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) jana jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa GEWE kutoka TGNP Mtandao, Matha Samwel akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa waliokuwa katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanahabari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za TAMWA Sinza Mori Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake jana jijini Dar es Salaam.
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na taasisi anuai za kijamii kimezinduwa tathmini ya ripoti juu ya utekelezaji wa mradi wa Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE).
Akizinduwa ripoti hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa jamii katika kujitambua na kuibua vitendo vya Ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari kuibua vitendo hivyo zaidi ya hapo awali.
Alisema idadi kubwa ya habari, makala na vipindi vya redio na televisheni juu ya masuala ya ukatili vimefanywa maeneo mbalimbali nchini, jambo ambalo limeonesha mafanikio ikiwa ni pamoja na jamii kuelewa zaidi masuala ya ukatili na unyanyasaji na wengine kuanza kuyapiga vita kwa ushirikiano.
Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA alisema mradi huo ulitekelezwa kwa pamoja kwa ushirikiano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Kituo cha Usuluhishi cha TAMWA (CRC), kinatekeleza mpango wa kutokomeza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE II) katika wilaya 10 za Tanzania bara na Zanzibar.
Kwa upande wake Matha Samwel Mratibu wa Mradi wa GEWE kutoka TGNP Mtandao, akizungumza alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kiasi cha kuibua changamoto ambazo zinaitaji utatuzi kwa ushirikiano na wadau wengine mbalimbali.
"...Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi wa GEWE kumekuwa na mafanikio makubwa, moja wapo kubwa ni kuanzishwa kwa vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya zote 10 za mradi, ambapo vituo hivyo vimekuwa vikitumika kama sehemu ya kutolea taarifa kwa jamii...sehemu ambayo wanajamii wanawake na wanaume wanakutana na kubadilishana taarifa na kuangalia namna ya kutatua matatizo yao yanayotoka katika jamii kama kubakwa, vipigo au kulawitiwa na mengineyo," alisema Bi. Samwel.
Hata hivyo aliongeza kuwa vituo vya taarifa na maarifa vimekuwa na msaada mkubwa katika maeneo hayo kwani jamii zimeweza kuvitumia pia kwa kujadili namna ya kukuza uchumi kwenye familia zao kwa kuanzisha vikundi vya kijasiriamali vinavyochangia pia kupunguza umasikini kwenye jamii suala ambalo linachangia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.
Anasema vituo vya taarifa na maarifa vimekuwa vikiunganisha nguvu na serikali na vyombo vingine vya dola kuhakikisha wanapambana na vitendo vya ukatili kwa kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake kwa watu wanaohusika ama kutuhumiwa na vitendo vya ukatili. Alitolea mfano katika eneo la Mwananyamala Kituo cha Taarifa na Maarifa kilishirikiana na Serikali kwa kuibua taarifa ya kuteswa kwa binti wa kazi za ndani na mwajiri wake jambo ambalo liliwezesha bosi huyo kufikishwa mahakamani.
"...Hivyo waweza kuona matokeo makubwa katika mradi wa GEWE ni kuanzishwa vituo vya taarifa na maarifa sehemu ambayo imekuwa ni kimbilio la wengi, na pili ni nguvu ya pamoja ya jamii katika uwajibikaji. Lakini changamoto iliyopo sasa ni namna ya kuwasaidia kwa kuwaifadhi waathiriwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii," alisema Mratibu huyo.
Aidha aliitaka Serikali na wadau wengine kujitokeza na kushirikiana katika kujenga kituo kikubwa cha kuwasaidi wananchi ambao wamekumbana na ukatili wa kijinsia wakati wakipatiwa huduma kabla ya kurejea katika jamii yao. "...Mfano kumekuwa kuna mabinti hata hapa Dar es Salaam wamekuwa wakikimbia kukeketwa na familia zao lakini hakuna sehemu ya kuwaifadhi, hivyo tunaiomba Serikali na wadau wengine wajitokeze ili kuunganisha nguvu tujenge kituo hiki," alisema.
No comments:
Post a Comment