Monday, December 22, 2014

BIASHARA 37,000 ZAANZISHWA KUPITIA MRADI WA UJASIRIMALI KWA VIJANA –ILO

001
Mratibu wa Mpango wa Ujasiriamali na Kukuza Ajira kwa Vijana ndani ya Shirika la kazi Duniani (ILO), Bw Mkuku Luis akitoa hotuba yake wakati akifungua mafunzo ya ujarimali kwa vijana yaliofanyika katika Desemba 19, 2014 jijini Dar es Salaam.
HABARI/PICHA NA PHILEMON SOLOMON FULLSHANGWEBLOG
002
Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa kitengo cha Mawasiliano (UNIC), Bi Usia Nkhoma Ledama akielezea zaidi kuhusiana na mafuzo hayo kwa vijana
003
Vijana mbalimbali kutoka mkoa wa Dar es Salaam wilaya zote tatu za mkoa wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo.
004
Mtoa mada Bw Ambokile Laurence akiwakilisha mada yake.
DSC_0039
Mratibu wa Mpango wa Ujasiriamali na Kukuza Ajira kwa Vijana ndani ya Shirika la kazi Duniani (ILO), Bw Mkuku Luis.
…………………………………………………………..
SHIRIKA LA Kazi Duniani (ILO) kupitia mradi wake wa mafunzo ya ujasirimali na kukuza ajira kwa vijana wameweza kutoa mafunzo yaliyoanzisha takribani biashara 37,000 za vijana nchini nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati ufunguzi wa mafunzo hayo ujasirimali kwa vijana, Mratibu wa Mpango wa Ujasiriamali na Kukuza Ajira kwa Vijana ndani ya Shirika la kazi Duniani (ILO), Bw Luis Mkuku amesema wana kuunga mkono juhudi za vijana wakufunzi ya kukuza uelewa wa ujasirimali kwa vijana wenzao nchini.
“leo tunatoa mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kupitia wakufunzi ambao ni vijana wenzao kuweza kuwafundisha na kuwatia moyo ili waweze kujikwamua katika dimbwi la umaskini kwa kuanzisha biashara zao,” aliongeza 
Amesema vijana mara nyingi kukutana na watu ambao wanawakatisha tamaa kuweza kufikia malengo na ndoto zao za kimaisha na mafunzo hayo yanatolewa na ILO ili kuweza kumwezesha kijana kufikia malengo yake maishani.
Mkuku alifafanua kwamba vijana wanaweza kuzikabili changamoto zao kwenye maisha yao ya kila siku kwa kuweza kufikiria jambo mbadala ikiwemo dhana ya kujitegemea kwa kuanzisha biashara zenye tija kwenye maisha yao.
Amesema kwamba tangu mafunzo hayo yaanze kutolewa na shirika hilo la kazi duniani ni miaka mitatu na wana wakufunzi wenye mbinu za ujasiriamali nchi nzima na kwa mkoa wa Dar es Salaam wana wakufunzi ishirini.
“vijana wengi wamekuwa na tatizo la kujiiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa sababu wanakosa watu wa kuwashauri jinsi ngani ya kuweza kujifunza stadi za maisha na kuanza maisha ya kujitegemea kwa ufupi ni kwamba vijana wanaopotea kwenye madawa ya kulevya ni vipaji vilivyopotea,” alisisitiza,
Kwa upande Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa kitengo cha Mawasiliano (UNIC), Bi Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba wameandaa mafunzo kwa vijana wasiokuwa mashuleni na walioko kwenye biashara.
Alifafanua kwamba mafunzo haya yanawalenga vijana wote wasio kuwa mashuleni na ambao waliokuwa katika matumizi ya madawa ya kulevya ili waweze kukabiliana na changamoto za kila siku za maisha.
“mafunzo yanahusisha vijana wote wa mkoa wa Dar es Salaam kutoka wilaya zote tatu za mkoa ni lengo la umoja wa mataifa kupambana na tatizo la umaskini kama malengo ya milenia yanavyosema,” amesema
Bi Ledama aliongeza kwamba mafunzo hayo pia yanahusisha vijana ambao pia wamo katika biashara lakini hapo mwanzo walifanya biashara bila kuwa na ufahamu au uelewa wa kutosha kuhusu biashara. 
Alifafanua kwamba mafunzo hayo yalianza miaka mitatu iliyopita na inalenga kumtoa kijana katika hali ngumu ya maisha ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya na kuweza kumwezesha kijana kujitegemea kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...