Friday, December 05, 2014

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR MAHMOUD THABIT KOMBO AFUNGA MAFUNZO YA SIKU 10 YA MFUMO WA UKUSANYAJI TAARIFA ZA AFYA

unnamedMratibu wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya (D.H.I.S) Suleiman Salum  Ali  akieleza mafanikio  ya mafunzo hayo  yaliyofanyika Hoteli ya Double Tree Nungwi, wa kwanza (kulia) ni Profesa Kristin Braa kutoka Chuo Kikuu cha Oslo ambao ni waandaaji wa mafunzo hayo kwa kushirikiana  na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wizara ya Afya Zanzibar. (kati) ni Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliefunga mafunzo hayo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar)unnamed1Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi cheti mmoja ya washiriki wa mafunzo ya D.H.I.S  Osama Al Zubair  kutoka Sudan wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi, Kaskazini Unguja.unnamed2Mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya D.H.I.S Mahmoud Thabit Kombo akiwahutubia washiriki wa mafunzo hayo kutoka Nchi za Afrika, Marekani, Ujerumani na Mashirika wahisani katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.unnamed3Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo alipokuwa akiyafunga mafunzo ya siku 10 yaliyofanyika Hoteli ya Double Tree Nungwi.unnamed4Mratibu wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya Suleiman Salum Ali akizungumza na waandishi wa Habari walioshiriki ufungaji wa mafunzo hayo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.unnamedPicha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya (D.H.I.S) wakiwa na mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar).

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...