Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani yanayoendelea nchini na namna Serikali kupitia Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ilivyojipanga kuhakikisha usalama wa ndege na abiria wanaotumia anga la Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) Bw. Charles Chacha akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa anga Tanzania na namna Tanzania ilivyofanikiwa kupunguza idadi ya ajali za ndege.
Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw. John Mayunga akifafanua utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa katika usafiri wa anga.Afisa mwongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Bi. Mossy Kitangita akiwahamasisha baadhi ya vijana na wanafunzi waliotembelea banda la maonesho la kitengo cha kuongozea ndege (hawapo pichani) kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kupata fursa ya kujiunga na fani ya uongozaji wa ndege ndani na nje ya nchi.Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, akimsikiliza Ofisa Utawala, kutoka Baraza la Ushauri la Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA-CC), Ms Catherine Monarya, wakati alipotembelea banda hilo kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo, Katibu Mkuu ameishauri taasisi hiyo kutoa elimu zaidi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, akimsikiliza Kaimu Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa katika Usafiri wa Anga na Maji kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya sekta ya Usafiri wa Anga, ambayo yanafanyika katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka(mwenye tai nyekundu), akimsikiliza Muongozaji Ndege katika kiwanja cha Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Bi. Mossy Kitang’ita, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), leo asubuhi katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka hiyo.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC), Bw. Nyello S. Abeid, akimueleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho, wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya sekta ya Usafiri wa Anga, ambapo maonesho hayo yameanza leo tarehe 3 na yataendelea mpaka tarehe 5/12/2014
No comments:
Post a Comment