Tuesday, December 16, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI SAMPULI ZA MADAWATI KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA MADARASA YA AWALI KATIKA MANISPAA YA LINDI MJINI.

unnamedMke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Gift Kyando mara baada ya kuwasili kwenye viwanja wa Shule ya Msingi Rahaleo iliyoko Manispaa ya Lindi Mjini kwa ajili ya kukabidhi sampuli za madawati aliyoyatoa kupitia taasisi yake kwenye Shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014unnamed1Sampuli za madawati yaliyotolewa na Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye Shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.unnamed2Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi kabla ya kukabidhi sampuli za madawati yaliyotolewa na Taasisi yake kwenye shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini kwenye sherehe fupi iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Rahaleo tarehe 15.12.2014.unnamed3Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikabidhi sampuli za madawati yaliyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Gift Kyando kwa ajili ya Shule za Msingi zenye madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Shule ya Msingi ya Rahaleo tarehe 15.12.2014.unnamed4unnamed5Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na binti Naida Seleman anayesoma darasa la awali katika Shule ya Msingi ya Rahaleo mara baada ya Mama Salma kukabidhi sampuli za madawati aliyoyatoa kwenye Shule za Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.unnamed6Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Lindi, wanafunzi wa madarasa ya awali wanaosoma katika Shule ya Msingi Rahaleo na walimu wao wakati wa sherehe ya kukabidhi sampuli za madawati tarehe 15.12.2014.
unnamed7Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Madarasa ya Awali katika Shule ya Msingi ya Rahaleo wakiwa pamoja na walimu wao wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati anawasili shuleni hapo tarehe 15.12.2014.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...