Wednesday, December 24, 2014

MASHAUZI CLASSIC KUTAMBULISHA WIMBO WAO MPYA “SURA SURAMBI

unnamed
Kundi zima la Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi, litafanya utambulisho wa wimbo wao mpya “Sura Surambi” kwa wakazi wa Morogogo Disemba 25 kwenye maadhimisho ya siku ya Christmas.
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhani maarufu kama Isha Mashauzi (pichani juu), ameuambia mtandao huu kuwa onyesho hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Savoy Hotel na watasindikizwa na mfalme wa kigodoro Msaga sumu.
Isha amesema “Sura Surambi” ni ngoma yao mpya kabisa iliyoachiwa mwishoni mwa mwezi uliopita na Morogoro unakuwa ndio mji wa kwanza baada ya Dar es Salaam, kuonjeshwa ladha ya wimbo huo ambao unafanya vizuri sana kwenye vituo vya radio.
“Huu ni utunzi na uimbaji wangu mimi mwenyewe, sina mengi ya kuongea zaidi ya kuwaahidi wakazi wa Morogoro burudani iliyokwenda shule,” alisema Isha.
Sura Surambi ni maandalizi ya albam mpya ijayo ya Mashauzi Classic ambapo tayari nyimbo mbili zimesharekodiwa, hii ikiwa ni pamoja na “Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzinga, binti wa waimbaji wakongwe wa taarab Abbas Mzinga na Bi Mwanamtama Amir.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...