Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuzungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alimpa taarifa Mheshimiwa Rais juu ya mafanikio ya ujenzi wa maabara katika Shule za Sekondari JIjini Dar es Salaam kwa asilimia 100% pamoja na matokeo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es salaam kwa asilimia 76% ukiacha mitaa miwili ambayo uchaguzi haukufanyika kwa sababu ya vurugu ambapo wahusika wote wanashughulikwa kisheria kutokana na vurugu walizosababisha.(Picha na Adam Mzee)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam ambao waliitika wito wa kumsikiliza wakati wa kulihutubia Taifa kupitia Wazee kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.( Picha na Adam Mzee
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba yake kwa Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ( Picha na Adam Mzee)

Baadhi ya Wanasiasa wakongwe waliohudhuria.
Kila wilaya ya mkoa wa Dar es salaam iliandaliwa sehemu maalum ya kukaa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Taifa kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alizungumzia uchaguzi na kutaka polisi kufanya kazi yao katika kuhakikisha uchaguzi ujao uchaguzi hauvurugwi na pia alifafanua mambo mbali mbali yaliyokuwa yakizungumziwa kuhusu akaunti ya ESCROW na kumwajibisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Ukumbi wa Diamond Jubilee ukiwa umefurika Wazee waliokuja kumsikiliza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Ukumbi ulifurika kila kona.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa ufafanuzi wa masula kadhaa yaliyoleta mkanganyiko kwenye sakata la Escrow Akaunti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akipanga makaratasi yenye hotuba yake wakati wa kuhutubia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.
Wananchi wakishangilia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhitimisha hotuba yake kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam.
Wananchi wakishangilia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhitimisha hotuba yake kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam.
Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru akimpongeza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kulihutubia taifa kwa kupitia wazee wa Dar es Salaam jana katika ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mbunge wa Kionondoni Iddi Azzan muda mfupi baadaya baada ya kulihutubia taifa kwa kupitia wazee wa Dar es Salaam jana katika ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment