Friday, September 05, 2014

ZIARA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KATIKA MRADI WA UNYAKUMI.







Picha zote kwa hisani ya kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa
*****************

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) kuhakikisha kuwa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa kwa ajili ya makazi zinakidhi mahitaji ya familia.
Balozi Seif Idd alitoa mwito huo mjini Singida mara baada ya kutembelea shughuli za ujenzi wa nyumba 20 katika eneo la Unyakumi, Manispaa ya Singida, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa nyumba 15,000 zinazojengwa na shirika hilo kote nchini kwa ajili ya makazi.
Alisema ingawa baadhi ya mashirika yamekuwa na nia njema ya kusaidia wananchi kumiliki nyumba kwa bei nafuu badala ya kuendelea kupanga, baadhi ya nyumba zinazojengwa ni ndogo kiasi cha kutokidhi mahitaji ya wanafamilia wanaonunua, wengi wao wakiwa wastaafu.
Kutokana na hali hiyo, Balozi Idd alisema kuwa ipo haja kwa Shirika hilo la Nyumba nchini kuhakikisha kuwa nyumba 15,000 zinazoendelea kujengwa kote nchini zinakuwa na ubora na viwango vinavyokidhi mahitaji ya familia.
Kaimu Meneja wa NHC Mkoa wa Singida, Peter Luheja alisema kuwa zaidi ya Sh milioni 900 zitatumika kugharimia ujenzi wa nyumba hizo 20 katika eneo la Unyakumi, Manispaa ya Singida.
Luheja alisema kuwa mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika Manispaa ya Singida unatarajiwa kukamilika na nyumba kuanza kuuzwa kwa wananchi ifikapo Oktoba mwaka huu.

SOURCE:HABARI LEO

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...