Tuesday, September 02, 2014

JK AFUNGUA BARABARA YA DODOMA-FUFU


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiraia ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km70.9) huku akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero kushoto pamoja na Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA, Ndugu Kuniaki Amatsu kulia huku Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa
barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km 70.9) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami. Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe pamoja na viongozi wengine 
 Taaswira ya mkeka mpya kutoka Dodoma hadi Fufu wa Kilomita 70.9 aliouzindua Rais Kikwete
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakimtazama Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA Ndugu Kuniaki Amatsu na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania bi Tonia Kandiero walipokuwa wakipanda mti kama ishara ya kumbukumbu
ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Fufu(Kilomita 70.9)
 Waziri wa zamani wa Ujenzi Mzee Job Lusinde akipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi wa rasmi wa barabara ya Iringa-Dodoma sehemu ya Dodoma-Fufu (Kilomita 70.9) huku Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli , Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge wakishuhudia tukio hilo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli  pamoja na viongozi wengine wakitaifa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma-Iringa sehemu ya Dodoma- Fufu Kilomita 70.9. Picha zote kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini –Wizara ya Ujenzi

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...