Wednesday, February 11, 2026

RAS ARUSHA ASISITIZA UTENDAJI KAZI UNAOZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dk. Toba Alnason Nguvila, amewasistiza watumishi wa Umma kufanya kazi kwa kufuata Sheria, taratibu na kanuni kwa kuzingatia kiwango cha juu cha Maadili ya Utumishi wa Umma, ili kufikia lengo la Serikali la kuwahudumia wananchi.

Dkt.Nguvila ametoa wito huo, wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa Umma mkoa wa Arusha, kwenye hafla fupi ya mapokezi yake, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, leo Februari 10, 2026, muda mfupi baada ya kupokelewa ofisini hapo, tayari kwa kuanza kutekeleza majukumu yake kwa washifa huo.

Amewasisitiza watumishi hao, kila mmoja kwa nafasi yake kuzingatia kuwa, mkoa huo ni mkoa wa Utalii hivyo wanalo jukumu la kuhakikisha wadau wa utalii wanafanya kazi kwenye mazingira rafiki, yasiyo na vikwazo vya aina yoyote huku akisisitiza kuto kuvumilia vikwazo vya kiutendaji wala urasimu unaokwamisha wawekezaji katika sekta ya utalii. 

“Sisi watalamu tunapaswa kuwa kichocheo cha kuiimarisha sekta ya utalii, kwa kuwa kila wilaya ina vivutio vyake, hivyo si busara kwa baadhi ya watendaji kuweka urasimu usio wa lazima unaoweza kudhoofisha sekta hiyo, sitavumilia urasimu wala migogoro inayokwamisha wawekezaji katika sekta ya utalii”. Amesema Dkt.Nguvila

Aidha, amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote, kutenga bajeti ya kutekeleza shughuli za utalii kwenye maeneo yao, kubuni vyanzo vya mapato pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato, ikiwa ni pamoja na kutoka maofisini na kuwafuata wananchi ili kubaini changamoto zao na kuzitatua kwa haraka.

Katika kutekeleza maelekezo ya Serikali, Dkt.Nguvila ameataka viongozi hao, kuwa na kampeni maalumu ya kutoa elimu na usajili sambamba na kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango wa Bima ya Afya kwa wote, ili ili kufikia lengo la Serikali ya awamu ya sita ya kila mwananchi kujiunga na Bima hiyo, itakayowawezesha kupata huduma za matibabu wanapougua.

Awali, Dkt.Nguvila amemshukuru Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumuanini na kumteua kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha na ameahidi kushirikiana na watalamu wa ngazi zote katika kuwahudumi wananchi.  







No comments:

RAS ARUSHA ASISITIZA UTENDAJI KAZI UNAOZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dk. Toba Alnason Nguvila, amewasistiza watumishi wa Umma kufanya kazi kwa kufuata Sheria, taratibu na kanun...