Saturday, February 14, 2026

RC CHALAMILA AENDELEA KUCHANJA MBUGA WILAYA YA KINONDONI







-Akagua utoaji huduma ya afya katika Hospitali ya Shifaa (Pan African Hospital Limited) Hospitali binafsi.

-Atinga Tandale akagua ujenzi wa shule ya ghorofa ya Sekondari Tarimba Abbas

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameendelea na ziara yake katika wilaya ya Kinondoni leo februari 12, 2026 ambapo amekagua kazi nzuri inayofanywa na sekta binafsi katika utoaji wa huduma ya afya hususani Hospital ya Shifaa iliyoko Hananasifu Kinondoni, ameridhishwa na uwekezaji uliofanyika katika hospitali hiyo na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kutenga maeneo yauwekezaji na kuwakaribisha watu binafsi kuwekeza kwa masilahi mapana ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Aidha RC Chalamila amekagua mradi wa elimu shule ya ghorofa ya Sekondari Tarimba Abbas yenye vyumba vya madarsa 21, Maktaba 1, vumba 3 vya maabara, Jengo la utawala, computer lab, na matundu 44 ya vyoo ambapo ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, huku akisisitiza maendeleo hayana chama hivyo amemshukuru Mhe Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa uwekezaji mkubwa katika sekta mbalimbali hapa nchini hususani sekta ya elimu.

Ifahamike kuwa Mhe Mkuu wa Mkoa yuko katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwa siku 3 katika Wilaya ya Kinondoni ambapo kesho tarehe 13, februari 2026 atasikiliza kero za wananchi katika eneo la Nyakasangwe na kuzipatia majawabu papo hapo hivyo usipange kukosa.

No comments:

RAIS SAMIA AONGOZA MJADALA WA MAJI NA MAENDELEO AFRIKA, AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ADDIS ABABA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendeleza diplomasia ya kimkakati kwa kushiriki Mkutano wa...