Friday, January 31, 2025

Rais Samia Suluhu Hassan Ashiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kwa Mjadala wa Usalama Mashariki mwa DRC

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika tarehe 31 Januari, 2025, katika ukumbi wa New Parliament Building, Harare, nchini Zimbabwe.

Mkutano huo unajadili hali ya ulinzi na usalama katika ukanda wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo viongozi wa nchi za SADC wanazingatia hatua za pamoja za kulinda amani na utulivu katika eneo hilo lenye changamoto za kiusalama.

Mkutano huu ni sehemu ya juhudi za SADC kuimarisha ushirikiano katika masuala ya usalama na kutafuta suluhu za kudumu kwa migogoro katika ukanda wa Afrika.

Thursday, January 30, 2025

KIKUNDI CHA UTAMADUNI CHA ILKIDING’A CHAFURAHIA UTALII WA IKOLOJIA PUGU KAZIMZUMBWI





Wageni kutoka Ilkiding’a Cultural Tourism Programme ya Arusha wametembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Pugu Kazimzumbwi jijini Dar es Salaam tarehe 29 Januari 2025, kwa lengo la kufurahia utalii wa ikolojia. Ziara hiyo imefanyika siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere tarehe 27-28 Januari 2025.

Kiongozi wa kikundi hicho, Eliakimu Laizer, amesema, “Tumefurahishwa sana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika utalii wa ikolojia hapa Pugu Kazimzumbwi. Tunawaasa wananchi wote kutembelea hifadhi za mazingira kama hii ili kufurahia uzuri wa asili na kujifunza umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.”

Ilkiding’a Cultural Tourism Programme imejipatia umaarufu kwa kucheza ngoma za asili za kabila la Maasai, na imekuwa kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi, ikipata mialiko mbalimbali ya kutumbuiza.

Hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi, inayojulikana kama “mapafu ya Dar es Salaam”, ni moja ya mabaki machache ya misitu ya pwani na ni muhimu kwa wakazi wa Dar es Salaam, Wilaya ya Kisarawe, na maeneo jirani.

SERIKALI YASIFU UJENZI WA BARABARA IRINGA, YATOA AGIZO KWA MKANDARASI ALIYECHELEWA







#Mkandarasi barabara ya Ilula Image-Ilambo atakiwa kurejea kazini mara moja

Iringa

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff, amesema serikali inaridhishwa na kazi zinayofanywa na wakandarasi wanaojenga barabara za Mtili – Ifwagi (Km. 14) na Wenda – Mgama (Km. 19) ambazo zinagharimu bilioni 52.

Barabara hizo zinajengwa chini ya mradi wa RISE, unaofadhiliwa kupitia mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia, ukiwa na lengo la kurahisisha usafirishaji wa mazao ya misitu, mboga mboga, chai, na mazao mengine kutoka mashambani hadi sokoni kwa wakati.

Akizungumza baada ya kuongoza kamati zinazohusika na usimamizi wa mradi huo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi, Mhandisi Seff amesema miradi hiyo ipo katika hatua nzuri na akawataka wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha kazi kwa wakati uliopangwa ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Aidha, amewataka wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya miradi kuwa walinzi wa kwanza wa barabara hizo ili kuzuia hujuma na wizi unaofanywa na watu wasio waaminifu, jambo ambalo limekuwa likisababisha hasara kwa serikali na kuhatarisha usalama wa miradi hiyo.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Seff ameagiza mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara ya Ilula Image – Ilambo (Km. 40) kurejea kazini mara moja ili kukamilisha kazi hiyo na kuondoa vikwazo vya mawasiliano vilivyopo kwenye barabara hiyo.

Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hii ili kuhakikisha wananchi wananufaika kwa wakati na miundombinu inaboreshwa kwa ufanisi.

Ngorongoro Conservation Area Shines at OTM India 2025: Discover Tanzania’s Ultimate Safari Experience!




The Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) is making waves at OTM India 2025, one of Asia’s leading travel and tourism trade shows! From January 30 to February 1, we invite you to visit our booth and explore the breathtaking beauty of Tanzania’s Ngorongoro Conservation Area (NCA)—a world-renowned safari destination that offers unmatched wildlife encounters and unforgettable cultural experiences.

Why Visit NCAA at OTM India 2025?

As one of Tanzania’s UNESCO World Heritage Sites, the Ngorongoro Conservation Area is home to the iconic Ngorongoro Crater, often called the Eighth Wonder of the World. It boasts an incredible concentration of wildlife, including the Big Five—lions, elephants, buffalos, rhinos, and leopards—as well as stunning landscapes that merge dramatic highlands, vast plains, and rich Maasai cultural heritage.

At our booth, visitors will:
Learn about unique safari experiences in the Ngorongoro Crater and surrounding areas.
Discover the diverse ecosystems that make this area a paradise for nature lovers and photographers.
Explore exclusive travel packages tailored for adventure seekers, honeymooners, and eco-tourists.
Engage with tourism experts who can guide you on planning a once-in-a-lifetime journey to Tanzania.

Ngorongoro: A Must-Visit Destination in Tanzania

Located in northern Tanzania, near Serengeti National Park, the Ngorongoro Conservation Area is a wildlife haven with over 25,000 animals roaming freely. The crater itself is the largest intact volcanic caldera in the world, offering a natural enclosure that supports an extraordinary ecosystem. Visitors can witness dramatic predator-prey interactions, take guided game drives, and experience authentic Maasai culture through village visits and traditional ceremonies.

Join Us at OTM India 2025!

Whether you’re a travel enthusiast, a tour operator, or a wildlife lover, our team at OTM India is ready to help you experience the magic of Ngorongoro. Don’t miss the opportunity to turn your safari dreams into reality—visit our booth from January 30 to February 1 and start your journey to Tanzania’s unforgettable landscapes and wildlife wonders.

📍 Location: OTM India 2025, Mumbai
📅 Dates: January 30 - February 1, 2025

🔗 Follow us on social media for updates and live highlights from the event!
#otmindia2025 #otmindia #visitngorongoro #unforgettableexperiences #ngorongorocrater #tanzaniaunforgettable

Rais Samia Awapongeza Washiriki wa Uokoaji Ajali ya Kuporomoka kwa Jengo Kariakoo


















Dar es Salaam, 30 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amewaandalia halfa ya chakula cha mchana washiriki wa zoezi la uokoaji wa ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika eneo la Kariakoo. Hafla hiyo imefanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kuthamini na kutambua juhudi kubwa zilizofanywa na vikosi vya uokoaji, taasisi mbalimbali, na wananchi waliojitokeza kusaidia katika operesheni hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia amepongeza mshikamano na uzalendo ulioonyeshwa na wadau wote waliohusika katika uokoaji, akisema kuwa kazi yao imeokoa maisha na kuleta matumaini kwa waathirika wa ajali hiyo. "Mmetimiza wajibu wenu kwa weledi, ujasiri, na moyo wa kujitolea. Taifa linawatambua na kuwathamini kwa mchango wenu mkubwa," alisema Rais Samia.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa serikali, maafisa wa vikosi vya uokoaji, madaktari, wahudumu wa afya, pamoja na wananchi waliojitolea kusaidia katika tukio hilo. Katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kuweka mikakati thabiti ya usalama wa majengo ili kuepusha ajali za aina hiyo kutokea tena nchini.

Aidha, hafla hiyo imepambwa na matukio mbalimbali, ikiwemo utoaji wa vyeti vya kutambua mchango wa washiriki wa uokoaji, hotuba za viongozi, na maonyesho mafupi ya picha zinazoonyesha juhudi za uokoaji.

Rais Samia amehitimisha hafla hiyo kwa kuwahakikishia waathirika wa ajali hiyo kuwa serikali itaendelea kutoa msaada wa karibu na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa ili kuepusha majanga kama haya siku zijazo.

 

LONGIDO WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA ELIMU YA FEDHA KUKUZA UCHUMI

Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Salum Kalli, akifungua mafunzo ya elimu ya fedha kwa wananchi, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Salum Kalli, akifungua mafunzo ya elimu ya fedha kwa wananchi, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha.
Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), akifafanua kuhusu umuhimu wa kutathmini mali kabla ya kuiweka dhamana, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha.
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akifafanua kuhusu umuhimu wa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha.
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Arusha Bi. Marietha Ngoma, akiwaelekeza wananchi jinsi ya kujiunga na kunufaika na huduma za Mfuko huo, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akifafanua kuhusu umuhimu wa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Longido, Arusha)


Na. Saidina Msangi, WF, Longido, Arusha.

Wananchi Wilayani Longido wamehimizwa kutumia fursa ya elimu ya fedha katika kuhakikisha kuwa wanapanga mipango ya biashara mapema ili kuweza kutumia vema mikopo inayotolewa na Serikali kupitia kila Halmashauri ili kujikwamua kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Salum Kalli, alipokuwa akifungua mafunzo ya elimu ya fedha, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka Taasisi na watoa huduma za Fedha ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha zilizo rasmi katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha.

Alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido imetenga kiasi cha Sh. milioni 25 kila mwezi kwa ajili ya mikopo ya kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu hivyo elimu ya fedha itawawezesha kupanga matumizi sahihi ya fedha hizo ili kukuza vipato vyao.

‘‘Tumieni fursa ya mafunzo haya ili kupata elimu sahihi kuhusu masuala ya fedha ikiwemo uwekezaji wa fedha, akiba na mikopo, kabla ya kuanza mipango ya kukopa fedha kutoka kwenye taasisi mbalimbali zinazotoa huduma hizo ili mikopo mnayochukua iwe na tija,’’ alisisitiza Mhe. Kalli.

Alisisitiza wananchi kuweka mipango thabiti ya biashara kabla ya kuchukua hatua za kukopa ili fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kurejesha mikopo hiyo kulingana na mikataba wanayoingia sambamba na kuchukua tahadhari ya wakopeshaji wasiofuata Sheria, kanuni na Taratibu.

‘‘Tumieni fursa ya elimu hii ya fedha mliyoipata kukuza biashara zenu endeleeni kuchapa kazi kwani nchi hii ina amani na utulivu, ulinzi na usalama hivyo fanyeni biashara kwa utulivu, elimu hii ikawe chachu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi hapa wilayani kwetu’’, alisisitiza Mhe. Kalli.

Aliwahimiza wananchi kutumia fursa ya kuishi mpakani mwa Tanzania na Kenya kufanya biashara kwa kufuata Sheria na Taratibu ikiwemo kupata leseni za biashara kuwawezesha kufanya biashara na nchi ya Kenya ili kukuza mitaji yao na uchumi kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Kalli aliwakumbusha wananchi wa Wilaya ya Longido kwa wale wenye utaratibu wa kutunza fedha nyumbani kuhakikisha kuwa wanafungua akaunti za benki na kutunza fedha kwa kuwa itawahakikishia usalama wa fedha zao.

Naye Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, alieleza kuwa ni muhimu kila mwananchi kuhakikisha kuwa kila anapopanga kuchukua mkopo awe na malengo ili fedha itakayopatikana itumike kwa utaratibu.

‘‘Unapotaka kuchukua mkopo hakikisha unachukua kwa ajili ya kitu cha msingi au kitu kinachozalisha kwani ni fedha ambayo lazima uirudishe baada ya muda fulani kwani mkopo sio zawadi,’’ alisisitiza Bw. Kibakaya.

Alisisitiza kuwa ni muhimu kukopa katika taasisi rasmi zilizosajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania na kuangalia riba ili kujiepusha na riba zisizofuata sheria, kanuni na taratibu ambazo ndio zinasababisha kuwa na mikopo inayojulikana kama kausha damu au mikopo umiza.

Naye Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, alisisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha kuwa kiwango cha fedha wanachopokea kiendane na mkataba wa mkopo huku wakiepuka kutumia kadi za benki kama dhamana.

‘’Ni muhimu kutumia sekta rasmi za fedha mnapochukua mkopo na kuhakikisha kuwa taasisi hizo zimesajiliwa kabla ya kupata huduma na pia kuomba hati ya kumaliza mkopo baada ya kurejesha mkopo husika ili kulinda dhamana zenu,’’alisisitiza Bw. Myonga.

Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na watoa huduma za Fedha inaendelea na programu ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido ambapo makundi ya wakulima, bodaboda, wafugaji, na wajasiriamali yanatarajiwa kufikishiwa elimu hiyo.

Monday, January 27, 2025

TUME YA MADINI YAAINISHA MIPANGO YA KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI







Uanzishwaji wa masoko ya madini wapunguza utoroshwaji wa madini

Elimu yatolewa kwa wachimbaji wadogo wa madini

CHUNYA

Ikiwa ni mkakati wa  kuhakikisha Tume ya Madini inavuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli la shilingi Trilioni Moja kwa mwaka 2024-2025 lililowekwa na Serikali, mikakati mbalimbali imeendelea kuwekwa na Tume ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa usimamizi katika masoko na vituo vya ununuzi wa madini nchini, utoaji wa leseni za madini na utoaji wa elimu kwa wachimbaji wadogo wa madini.

Hayo yamesemwa leo Januari 27, 2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Leseni na TEHAMA, Mhandisi Aziza Swedi kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wachimbaji wa madini katika mikoa ya kimadini ya Chunya na Songwe yaliyofanyika Chunya Mjini.

Amesema kuwa, kwa kutambua mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo wa madini nchini, Serikali kupitia Tume ya Madini imepanga kuwapatia elimu kuhusu uchimbaji salama na endelevu sambamba na kuwaunganisha na Taasisi za Kifedha na kupata mikopo ili uchimbaji wao uwe na manufaa huku Serikali ikipata kodi na tozo mbalimbali.

“Sambamba na kuhakikisha wachimbaji wadogo wa madini wanaendelea kunufaika bila kuathiri mazingira, suala la usalama kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ni endelevu na tumelipa kipaumbele ambapo kwa sasa tumeendelea kutoa mafunzo katika mikoa mbalimbali ikiwepo mikoa ya kimadini ya Songwe na Chunya,” amesema Mhandisi Swedi.

Akielezea mchango wa  wachimbaji wa madini kwenye Sekta ya Madini, Mhandisi Swedi ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini  mwaka 2019, kasi ya utoroshaji wa madini imepungua nchini kwa kuwa wachimbaji wadogo wa madini kwa sasa wanauza madini yao katika masoko na vituo vya ununuzi wa madini hivyo kupelekea makusanyo ya maduhuli kuongezeka.

“Kwa mfano kati ya kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba, 2024 katika mwaka wa fedha 2024-2025 mkoa wa kimadini wa Chunya umekusanya kiasi cha shilingi bilioni 30 sawa na asilimia 50 ya makusanyo ya shilingi bilioni 60 katika mwaka wa fedha 2024-2025.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Swedi amewataka wachimbaji wa madini kuwa wazalendo kwa kulipa kodi na tozo mbalimbali sambamba na kufuata Sheria za Madini na Kanuni zake.

Naye Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Mhandisi Hamisi Kamando ameongeza kuwa lengo la Tume ya Madini kutoa mafunzo hayo hasa kwenye masuala ya usalama kwenye shughuli za madini ni kuhakikisha kuwa uwepo wa migodi ya madini hauathiri afya na mazingira kwa wachimbaji na jamii inayozunguka.

“Sisi kama wataalam kutoka Tume ya Madini tunatamani kuona wachimbaji wa madini wanaendesha shughuli zao kwa kufuata Sheria na Kanuni za Mazingira na kuepusha ajali zinazoweza kutokea na kupoteza nguvu kazi ya nchi.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga pia kukusanya maoni na kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wa madini na kuendelea kuvutia ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini.

Wakati huohuo wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo wamepongeza  uwepo wa mafunzo na kusisitiza elimu hii kuendelea kutolewa kwenye majukwaa, makongamano na maonesho mbalimbali.

Mashaka Fungameza ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu katika eneo la Chunya mkoani Mbeya amesema kuwa, uwepo wa mafunzo hayo utawawezesha kuboresha shughuli za uchimbaji wa madini kwa kuzingatia kanuni za usalama na kupunguza ajali zinazoweza kujitokeza hasa kipindi cha mvua na kupunguza vifo.

Naye Masunga Mapalala kutoka kampuni ya Apex Resources Limited kutoka Chunya amewataka wachimbaji wa madini kutumia elimu inayotolewa na Tume ya Madini kwa kuimarisha usalama kwenye shughuli za uchimbaji wa madini.

Mada zinazotolewa katika mafunzo hayo ya siku mbili yanayotarajiwa kumalizika kesho Januari 28, 2025 ni pamoja na  Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, kanuni zake na mabadiliko yake ya mwaka 2017; utoaji na usimamizi wa leseni za madini;  afya na usalama kwenye migodi na utunzaji na uhifadhi wa mazingira migodini.

Mada nyingine ni pamoja na biashara ya madini na masoko, usimamizi wa fedha na kodi, ushirikishwaji wa watanzania katika shughuli za madini

DKT. BITEKO AFUNGUA MKUTANO WA NISHATI BARANI AFRIKA 2025




Dar es Salaam, Januari 27, 2025 — Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Doto Biteko, leo ameongoza hafla ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Nishati Barani Afrika (Africa Energy Summit 2025). Mkutano huo unaendelea kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, ukihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Dkt. Biteko aliainisha umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika kushughulikia changamoto za upatikanaji wa nishati endelevu barani Afrika. Alisisitiza kuwa mkutano huu ni jukwaa muhimu la kubadilishana mawazo na uzoefu kwa lengo la kuimarisha sekta ya nishati na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa bara zima.

“Mkutano huu unatoa nafasi ya kujadili mikakati ya pamoja ya kuongeza upatikanaji wa nishati safi, nafuu, na endelevu kwa wote. Afrika ina rasilimali nyingi, na kwa kushirikiana, tunaweza kuzitumia kuwanufaisha watu wetu,” alisema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Nishati, Mha. Felchesmi Jossen Mramba, alisisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kutekeleza miradi mikubwa ya nishati ambayo itaboresha upatikanaji wa umeme na kupunguza utegemezi wa vyanzo vya nishati visivyohifadhi mazingira.

Mkutano huu, ambao umeleta pamoja viongozi wa kisiasa, wataalam wa nishati, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, na wadau wa sekta binafsi, utadumu kwa siku tatu. Mada kuu zinazojadiliwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa, uwekezaji katika vyanzo vya nishati jadidifu, na usimamizi wa miradi mikubwa ya nishati barani Afrika.

Mkutano wa Nishati Barani Afrika (Africa Energy Summit) umeonekana kuwa jukwaa la kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya nishati, huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa tukio hili muhimu kwa mara ya kwanza.



WAKANDARASI WANAOJENGA BARABARA ZA TACTIC JIJINI ARUSHA KAMILISHENI UJENZI KWA WAKATI* MHANDISI MATIVILA

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila ameagiza wakandarasi wanaojenga barabara za...